Home SPORTS YANGA YATINGA FAINALI SHIRIKISHO

YANGA YATINGA FAINALI SHIRIKISHO

Na: TIMA SULTAN

MABINGWA wa Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga SC wamefanikiwa kutinga hatua ya fainali za mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF Confederation Cup).

Historia hiyo imeandikwa leo nchini Afrika Kusini kwa Wanajangwani hao kufanikisha kutinga hatua hiyo wakiichapa Marumo Gallants ya nchini huko mabao 2-1.

Kwa ushindi huo Yanga SC wanaingia fainali kifua mbele wakiwa na kifuko chenye jumla ya mabao 4.

Mabao 2 waliyapata kwenye mchezo wao wa awali ambayo yaliingizwa kimiani na Azizi Ki pamoja na Benard Morrison huku 2 ya leo yakifungwa na Fiston Mayele pamoja Kennedy Musonda.

Ikumbukwe kwamba Yanga ni timu ya pili kuingia kwenye fainali kwa timu za Tanzania, ya kwanza ilikuwa ni Simba ambayo ilitinga hatua hiyo mwaka 1993 lakini jina la mashindano likiwa tofauti

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here