Home LOCAL SERIKALI KUTOWAFUMBIA MACHO WATENDAJI WANAOKWAMISHA JITIHADA ZA RAIS SAMIA 

SERIKALI KUTOWAFUMBIA MACHO WATENDAJI WANAOKWAMISHA JITIHADA ZA RAIS SAMIA 

Serikali imesema haitawafumbia macho watendaji wa sekta ya afya wanaokwamisha jitihada za Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika maboresho sekta ya afya.

Akizungumza katika kikao kazi cha watendaji hao wa Kanda ya Ziwa kwa mikoa mitano ya Mwanza,  Simiyu, Mara Geita na Shinyanga na Bohari ya Dawa (MSD), Katibu Tawala wa Mara Msalika Makungu, alisema lengo la Rais Dk.Samia kufanya maboresho ya sekta hiyo ni kumpatia huduma bora mwananchi hivyo watendaji watambue wajibu walionao katika kufanya kazi kwa weledi na kumsaidia kufikia lengo la maboresho hayo.

Alisema Kanda hiyo haitawafumbia macho watendaji wanaokwamisha jitihada hizo kwa makusudi.

Alisema, kikao kazi hicho ni muhimu kwa watendaji kuwakumbusha wajibu walio nao katika kufanya kazi kwa weledi na kuwa sehemu ya mabadiliko kwa kutoa huduma nzuri kuanzia katika mapokezi ya wagonjwa, lugha na kuwa na matumizi sahihi ya dawa na vifaa tiba.

“Ni muhimu wataalamu watimize majukumu yao kwa weledi na huduma ziwafikie wananchi kwa kuwa sekta ya afya ni sekta mtambuka yenye tija katika utekelezaji wa malengo ya mpango wa serikali kijamii na kiuchumi,”alisema.

Kwa upande wake Meneja wa Kanda hiyo wa MSD, Egidius Rwezaura, alisema hivi karibuni wanatarajia kupokea vifaa vya afya zikiwemo  dawa na vifaa tiba aina 100 ikiwemo vitanda na mshine za maabara ambavyo vitamaliza changamoto ya mahitaji yaliyopo.

Pia alisema mkakati ni kuwapo vifaa vingine vingi vya akiba katika bohari, kufikia lengo la Rais Dk. Samia katika  maboresho ya huduma sekta ya afya nchini.

Naye Mfamasia Mratibu Kiongozi wa Huduma za Bidhaa za Afya kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mathew Mganga, alisema watendaaji hao watambue kuwa Rais ametoa fedha nyingi za dawa na vifaa ni vyema zitumike katika ununuzi wa bidhaa hizo na sio matumizii mengine.

Alisema lengo la maboresho sekta hiyo, ni kufanikisha huduma bora kwa wananchi ambapo bado fedha zinazomiminika na hatua zilizochukuliwa na serikali ya Rais Dk.Samia haiendani na huduma bora wanazopatiwa wananchi hivyo ni lazima kuchukua hatua.

Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mara Dkt Zabron Masatu, alisema wamepokea maelekezo hayo wataenda kubanana ndani katika utendaji kuweza kufikia lengo la Rais katika maboresho ya huduma bora za afya kwa wananchi.

Previous articleDKT. MPANGO AVUTIWA NA UBUNIFU WA PROGRAMU YA IMBEJU KATIKA KUCHOCHEA UJUMUISHI WA UCHUMI NCHINI
Next articleNCHI 14 NA MAKAMPUNI  ZAIDI YA 1000 YATHIBITISHA KUSHIRIKI MAONESHO YA SABASABA MWAKA HUU
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here