Lift hiyo imeporomoka mapema leo Mei 24, 2023 ambapo taarifa za awali zinaeleza kuwa lift hiyo iliyokuwa na zaidi ya watu saba ndani yake, imeporomoka kutoka ghorofa kati ya kumi hadi 14, na kupeleka majeruhi sana wa viungo. akufikishwa katika hospitali ya Kairuki kwa ajili ya matibabu.
RC Chalamila baada ya kufika eneo la tukio nakushuhudia majeruhi katika hospitali ya kairuki ametoa maagizo kwa vyombo vya usalama kufanya uchunguzi wa kina wa tukio hilo pamoja na kuwataka wamiliki wa majengo marefu kufanya ukaguzi wa mara kwa mara wa lift za majengo yao.
Wakati huo huo Kwa mujibu wa Mwakilishi wa Kamanda wa Jeshi la Zimamoto Mkoa wa Kinondoni, Mrakibu Peter Mtui wakati akitoa taarifa mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam aliyefika eneo hilo, amesema taarifa za awali zinaonesha kuwa lift hiyo ilikuwa kwenye majaribio baada ya kufanyiwa matengenezo na ilitumika kinyume na utaratibu.
Msimamizi wa Millenium Tower, Martin Mhina amesema lift hiyo iliwekewa utepe kwa ajili ya kuzuia watu wasipande lakini waliukata na kuitumia bila ruhsa ya wasimamizi katika jengo hilo.
Ripoti zinasema Majeruhi katika ajali hiyo ya Lift walikimbizwa katika hospitali ya Kairuki Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya matibabu katika kitengo cha kifupa.