Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi, Wakuu wa Taasisi mbalimbali pamoja na Wananchi waliohudhuria hafla ya utiaji saini Mikataba ya kupeleka Huduma za Mawasiliano Vijijini kati ya Serikali na Makampuni ya Simu iliyofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma
Viongozi mbalimbali, Wakuu wa Taasisi, Wabunge pamoja na Wananchi wakiwa kwenye ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete kwa ajili ya kushuhudia hafla ya utiaji saini Mikataba ya kupeleka Huduma za Mawasiliano Vijijini kati ya Serikali na Makampuni ya Simu (TTCL, Vodacom, Airtel, Halotel, Tigo) iliyofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma
Msanii Mrisho Mpoto akitumbuiza katika hafla ya utiaji saini Mikataba ya kupeleka Huduma za Mawasiliano Vijijini kati ya Serikali na Makampuni ya Simu (TTCL, Vodacom, Airtel, Halotel, Tigo) iliyofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea zawadi ya Kishkwambi chenye maelezo mbalimbali ya Minara ya Simu kutoka kwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye wakati wa hafla ya utiaji saini Mikataba ya kupeleka Huduma za Mawasiliano Vijijini kati ya Serikali na Makampuni ya Simu (TTCL, Vodacom, Airtel, Halotel, Tigo) iliyofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa pamoja Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye wakati akisikiliza maelezo ya Mifumo mbalimbali ya Mawasiliano nchini mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete kwa ajili ya kushuhudia hafla ya utiaji saini Mikataba ya kupeleka Huduma za Mawasiliano Vijijini kati ya Serikali na Makampuni ya Simu (TTCL, Vodacom, Airtel, Halotel, Tigo) iliyofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa Makampuni ya simu kubuni teknolojia ya gharama nafuu itakayowezesha kila Mtanzania kupata huduma ya mawasiliano popote alipo nchini.
Rais Samia ametoa wito huo leo wakati wa utiaji saini mikataba ya upelekaji huduma za mawasiliano nchini kati ya Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) na watoa huduma za mawasiliano uliofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete.
Aidha, Rais Samia ameyataka Makampuni hayo kuleta teknolojia inayoendana na mazingira ya Tanzania kwa kuwa zipo changamoto zinazotokana na hali ya kijiografia na kipato kidogo cha wananchi katika baadhi ya maeneo.
Rais Samia pia amewataka Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA) kushirikiana na UCSAF na wakandarasi kuhakikisha njia zinapitika katika maeneo ya vijijini inapokwenda kujengwa minara hiyo.
Hali kadhalika, Rais Samia amewataka Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kuhakikisha kuwa minara inayokwenda kujengwa vijijini inapelekewa umeme ili faida inayokusudiwa ipatikane haraka.
Aidha , Rais Samia amesema kuwepo kwa huduma bora za mawasiliano hususan katika maeneo ya vijijini ni muhimu sana kiuchumi, kisiasa, kijamii, kiutamaduni na hata katika masuala ya ulinzi na usalama wa nchi yetu.
Miradi miwili iliyotiwa saini ni ya ujenzi wa minara 758 katika Kata 713 wenye gharama ya Shilingi bilioni 265.3 pamoja na mradi wa kuongeza uwezo wa minara 304 ya mawasiliano utakaogharimu kiasi cha Shilingi bilioni 10.2.
Kwa upande wake Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amezitaka kampuni za mawasiliano hapa nchini kuendelea kuwekeza na kuongeza mitaji ya uwekezaji wao ili kuimarisha mawasiliano nchini.
“Nitoe wito kwa kampuni za mawasiliano Tanzania kuwa serikali itaendelea kuwapa ushirikiano wakati wote ili kuhakikisha suala la mawasiliano linaimarika na muendelee kuwekeza, endeleeni kuweka mitaji zaidi msiwe na mashaka Tanzania ya Dkt Samia Suluhu Hassan iko vizuri na itaendela kushirikiana na nanyi.”
Naye Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Tulia Ackson amempongeza Rais Samia kwa hatua ya kurejesha Tume ya Mipango ambayo itasaidia Taifa kusonga mbele kwa kuunganisha sekta mbalimbali na maendeleo yanapoenda kwa wananchi sekta zikiwa zinatazamana.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye amesema kuwa Serikali imeendelea kushirikiana na wadau ili kusaidia Watanzania kutumia fursa zinazotokana na huduma za mawasiliano ikiwemo za kidigitali.
“Hadi sasa USCAF imeingia makubaliano na kampuni za kufikisha huduma za mawasiliano katika kata 1,258 zenye jumla ya vijiji 3,704 na wakazi milioni 15.1, jumla ya minara ya mawasiliano 1,380 itajengwa aidha katika mikataba 19 ambayo UCSAF imeingia na watoa huduma za mawasiliano,”amesema Waziri Nape.
Aidha, ameongeza kuwa Serikali imetoa ruzuku ya shilingi bilioni 199.9 na ni ushahidi wa jinsi Serikali inavyothamani na kuhakikisha kuwa watanzania hasa wa vijijini wanapata huduma za mawasiliano.
Awali Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF),Bi. Justine Mashiba amesema katika kutekelza miradi hiyo, UCSAF ilitangaza zabuni katika maeneo 763 na baada ya mchakato wa zabuni yamepatikana maeneo katika kata 713 ambako minara 758 itakwenda kujengwa huku ushiriki wa watoa huduma.
Aidha amewataja watoa huduma ambao watashiriki katika kujenga minara hiyo kuwa ni TTCL ambayo inajenga minara 104 katika kata 104, Vodacom Tanzania itajenga minara katika kata 190 , Airtel Tanzania itajenga minara 168 katika kata 161, MIC Tanzania imeshinda zabuni ya kujenga minara 262 katika kata 244, pamoja na Halotel ambayo imeshinda kata 34 na itajenga minara 34.
“Mbali na kujenga minara hiyo pia tunakwenda kuongeza nguvu minara 304 ambayo ilikuwa inatoa teknolojia ya 2G na sasa itakwenda kutoa teknolojia ya 3G na baadhi ya maeneo itatoa teknolojia ya 4G”. amesema Bi. Justina.
Hata hivyo amefafanua kuwa katika kuongeza nguvu ya minara hiyo, MIC Tanzania itaongeza nguvu katika minara 148, TTCL minara 55, Airetel minara 32 Vodacom Tanzania minara 69.