Home BUSINESS BRELA YATOA ELIMU YA BIASHARA KWA WANAFUNZI CHUO KIKUU CHA KIISLAMU

BRELA YATOA ELIMU YA BIASHARA KWA WANAFUNZI CHUO KIKUU CHA KIISLAMU

Wanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Kiislamu Morogoro(MUM), wametakiwa kukabiliana na changamoto za ajira, mara baada ya kuhitimu masomo yao kwa kufanya biashara na kuzirasimisha Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni ( BRELA).

Rai hiyo imetolewa na Afisa Usajili wa BRELA Bw. Lumambo Shiwala wakati akiwasilisha mada kuhusu Usajili wa majina ya Biashara na Makampuni kwa wanafunzi wa chuo hicho, waliofanya ziara ya mafunzo katika ofisi za BRELA tarehe 17 Mei, 2023, jijini Dar es Salaam.

Wanafunzi hao wa mwaka wa Pili ngazi ya Diploma ya Sheria na Usimamizi wa Biashara wamehamasishwa kwa kuhakikisha kuwa baada ya kuhitimu masomo yao wakabiliane na changamoto ya ukosefu wa ajira kwa kuanzisha biashara na kuzirasimisha BRELA ambazo zitawawezesha kupata fursa za mikopo kutoka taasisi mbalimbali za fedha.

Aidha, Bw. Shiwala amesema kuwa Usajili wa Majina ya Biashara, Makampuni, Alama za Biashara na Huduma, pamoja na Utoaji wa Leseni za Biashara Kundi “A” na Leseni za Viwanda zote zinazosimamiwa na kulindwa na BRELA, zinafanyika kwa njia ya mtandao, lengo likiwa ni kuokoa muda na kupunguza gharama.

Kwa upande wake Mhadhiri kutoka Chuo hicho Bw. Habibu Siraji, ameishukuru BRELA kwa elimu waliyoipata na kuahidi kuwa mabalozi wazuri wa BRELA.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here