Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Delilah Kimambo akimkabidhi Afisa Uuguzi Danny Hakorimana kutoka Hospitali ya King Faisal iliyopo jijini Kigali nchini Rwanda cheti cha kuhitimu mafunzo ya jinsi ya kuwahudumia wagonjwa mahututi na dharura . Kozi hiyo ya miezi sita ilihudhuriwa na washiriki 22 kutoka nchini Rwanda na Hospitali mbalimbali za hapa nchini.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Delilah Kimambo akimkabidhi Afisa Uuguzi Masoud Mheruka kutoka Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) iliyopo jijini Dodoma cheti cha kuhitimu mafunzo ya jinsi ya kuwahudumia wagonjwa mahututi na dharura. Kozi hiyo ya miezi sita ilihudhuriwa na washiriki 22 kutoka nchini Rwanda na Hospitali mbalimbali za hapa nchini.
Mratibu wa Mafunzo ya jinsi ya kuwahudumia wagonjwa mahututi na dharura ambaye pia ni Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Joshua Ogutu akieleza jinsi mafunzo hayo yalivyofanyika wakati wa hafla fupi ya kufungwa kwa mafunzo hayo ya miezi sita iliyofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.
Afisa Uuguzi Bizimana Theodore kutoka Hospitali ya King Faisal iliyopo jijini Kigali nchini Rwanda akitoa neno na shukrani wakati wa hafla fupi ya kufungwa kwa mafunzo ya miezi sita ya jinsi ya kuwahudumia wagonjwa mahututi na dharura. Mafunzo hayo yalihudhuriwa na washiriki 22 kutoka nchini Rwanda na Hospitali mbalimbali za hapa nchini.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya jinsi ya kuwahudumia wagonjwa mahututi na dharura yaliyotolewa na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakikata keki wakati wa hafla fupi ya kufungwa kwa mafunzo hayo ya miezi sita iliyofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Delilah Kimambo akimlisha keki ya kumpongeza mkufunzi wa mafunzo ya jinsi ya kuwahudumia wagonjwa mahututi na dharura ambaye pia ni Afisa Uuguzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Samweli Mpiga wakati wa hafla fupi ya kufungwa kwa mafunzo hayo ya miezi sita iliyofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.
Picha na Khamisi Mussa