Home SPORTS SIMBA YAILAZA WYDAD CASABLANCA 1-0 KWA MKAPA

SIMBA YAILAZA WYDAD CASABLANCA 1-0 KWA MKAPA

Na: Tima Sultan

KIKOSI cha wekundu wa Msimbazi, Simba SC leo kimeibuka na Ushindi wa bao 1_0 dhidi ya Wydad AC mchezo uliochezwa leo majira ya saa 10:00 jioni katika Dimba la Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Wekundu hao wa Msimbazi wameibuka naushindi huo wakiwa ndio wenyeji wa mchezo.

Mgeni rasmi kwenye mchezo huo akiwa ni Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Tulia Akson.

Miongoni mwa viongozi wa Simba waliohudhuria mchezo huo nimwekezaji wa klabu hiyo Mohammed Dewj.

Mchezo huo ni wakwanza kwenye hatua ya Robo Fainali na wanatarajia kurudiana mwishoni mwa wiki ijayo nchini Morocco.

Katika kipindi cha kwanza cha Mchezo simba walikuwa hatari zaidi kwakufika kwenye maeno ya hatari ya timu pinzani na Dakika ya 31 Jean Baleke aliipatia timu yake bao la kuingoza.

Katika kipindi hicho cha kwanza Wydad wamejaribu kufanya mashambulizi lakini hayakuzaa matunda na timu zilikwenda mapumziko simba wakiwa mbele kwa bao hilo.

Kipindi cha Pili cha mchezo huo Simba SC waliendelea kupambana kuhakikisha wanalinda bao lao lililodumu hadi mwisho wa mchezo huo

Kikosi cha Simba kilichoanza ni: Ally Salim, Shomari Kapombe, Henock Inonga, Dennis Onyango, Mohammed Hussein, Muzamiru Yassin, Sadio Kanoute, Kibu Dennis, Saido Ntibazonkiza, Clatous Chama na Jean Baleke

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here