Home LOCAL MAAMBUKIZI UGONJWA WA MALARIA TANZANIA YASHUKA

MAAMBUKIZI UGONJWA WA MALARIA TANZANIA YASHUKA

kaimu meneja mpango wa Taifa wa kudhibiti Maleria kutoka Wizara ya Afya Dkt. Abdallah Lusasi akizungumza kwenye Semina ya siku moja ya waandishi wa habari iliyofanyika leo April 21, 2023 Jijini Dar es Salaam Baadhi ya Maafisa wa Serikali na Waandishi wa habari wakimsikiliza kt. Abdallah Lusasi Alipokua akizungumza katika Semina hiyo.

(PICHA NA: HUGHES DUGILO)

NA: HUGHES DUGILO, DAR ES SALAAM

Katika kuelekea maadhimisho ya siku ya maleria Duniani, Serikali ya Tanzania imejipanga kuja na mipango ya afua za kukabiliana na ugonjwa huo ikiwemo kuanza kutoa Dawa kinga kwa watoto wa shule za msingi ili kufikia malengo ya maambukizi kwa asilimia 0.

Akizungumza kwenye Semina ya siku moja ya waandishi wa habari iliyofanyika leo April 21, 2023 Jijini Dar es Salaam kuelekea katika maadhimisho ya siku ya Maleria Duniani tarehe 25 April,2023 Jijini humo, kaimu meneja mpango wa Taifa wa kudhibiti maleria kutoka wizara ya Afya Dkt. Abdallah Lusasi amesema hali ya maambukizi, vifo, pamoja na wagonjwa wanao lazwa kutokana na ugonjwa wa maleria imeshuka na kuonesha mafanikio makubwa katika kuelekea mpango wa kuondosha ugonjwa huo ifikapo mwaka 2030.

Ameeleza kuwa pia kuna mikakati zaidi ya kupambana na Marelia ikiwemo upatikanaji wa Dawa na vyandarua, kupitia kitengo cha kampeni ya mapambano dhidi ya Marelia na kitengo cha utafutaji fedha na usimamizi wa miradi ya Marelia.

“Hali ya Tanzania kwa Sasa hivi ni asilimia 94 wapo kwenye hali tofauti za maambukizi lakini tulipotoka mwaka 2017 ilikuwa ni asilimia 7.5 ya maambukizi, dhamira yetu ni kufika asilimia 3.5 mwaka 2025, Sasa tupo wapi tutasema mbele.

“Mikakati ambayo tumejiwekea kwa sasa ni miwili ikiwemo wa kwanza ni kuhakikisha tunapunguza wingi wa maambukizi na wa pili ni kutokomeza maleria,” amesema Lusasi.

Nae Mratibu wa Udhibiti wa Maleria Mkoa wa Dar es Salaam Dkt. Ford Chisongela, amesema kuwa katika mkoa huo licha ya kuwa ni miongoni mwa mikoa inayofanya vyema katika kudhibiti maleria bado wana hitaji kuja na afua za kukabiliana na ugonjwa huo ikiwemo kugawa vyandarua kwa watu wasiojiweza ili kuhimiza matumizi ya vyandarua.

“Tuko asilimia 0.7 sawa na Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Dodoma, Iringa na Njombe, kwa hiyo tumepiga hatua sana lakini moja ya mambo ambayo yametuwezesha kufika huko ni matumizi ya vyandarua.

“Dar es Salaam ilianza kunyunyizia viuwadudu kwenye mazalia ya mbu mwaka 1996. Mikoa mingine wameanza miaka mitatu iliyopita hii imesaidia kupunguza kiwango cha maleria pamoja na matibabu ambayo tunawapa wananchi wetu.

“Ukiangalia Kiwilaya Ilala inaongoza kuwa na Maleria, Kimkoa tukiwa na asilimia 0.7 wenzetu Ilala wana asilimia 1.7, kwa hiyo wao ndio wanaongoza wakifatiwa na Kinondoni na Ubungo ambazo Takwimu zao zinafanana, kisha Tameke na Kigamboni wao wana maambukizi kidogo,”amemaliza Chisongela.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Rashid Mfaume amesema mkoa huo upo tayari kwa maadhimisho ya kitaifa ya malaria huku akiainisha mipango katika kuahakikisha inapunguza maambukizi kwa kata ya Msongora Ilala, na tungi Kigamboni, ambazo bado zina maambukizi ya juu licha ya kuwa miongoni mwa mikoa tisa iliyo chini kwa maambukizi ya ugonjwa huo.

Maadhimisho ya siku ya Maleria Duniani mwaka huu yatafanyika April 25 katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam yakiwa na Kaulimbiu isemayo ‘WAKATI WA KUTOKOMEZA MALERIA NI SASA, BADILIKA, WEKEZA, TEKELEZA’

#ZIROMALERIAINAWEZEKANA

(Picha za matukio mbalimbali katika Semina hiyo)

Previous articleMKURUGENZI WA MSAMA PROMOTIONS ALEX MSAMA ALAZWA JKCI
Next articleTUSHEREHEKEE SIKUKUU YA EID EL FITR KWA AMANI NA UTULIVU ‘ DISKO TOTO HAPANA”
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here