CHAMA Cha Mapinduzi (CCM)kupitia Katibu Mkuu wake Daniel Chongolo kimesema kwamba Serikali haiwezi kuendelea kuona mkulima wa ndani anaumia lakini wakulima wa nje ya Tanzania wakinufaika.
Ametumia nafasi hiyo kuelezea kuwa Chama hicho pia kitatafuta ufumbuzi wa kudumu wa suala la Mafuta ya alizeti kushuka bei wakati kuna gharama kubwa za uzalishaji wa Mafuta hayo .
Chongolo amesema hayo leo Machi 4,2023 akiwa kwenye ziara yake mkoani Singida yenye lengo la kusikiliza na kutatua changamoto za wananchi sambamba na kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi Mkuu ambayo inaendelea kutekelezwa.
Akiwa kwenye ziara hiyo Chongolo amepokea malalamiko ya wakullima wa alizeti kuhusu kushuka kwa bei ya Mafuta ya alIzeti ambapo baada ya malalamiko hayo ameahidi Serikali ya Chama hicho itatafuta ufumbuzi wa kudumu.
Baadhi ya hatua ambazo zinapaswa kuchukuliwa kwa mujibu wa Chongolo ni pamoja kulishughilikia suala hilo kwa kuishauri Serikali irejeshe kodi ya mafuta ya kula iliyokuwa imefutwa.
“Kwa sasa siwezi kulitolewa maelezo mengi, niachieni mimi kwa Sababu ninalimudu, Serikali haiwezi kumnufaisha mkulima wa nje wakati wakulima wetu wanaumia.”
Kabla ya Katibu Mkuu Chongolo kutoa maelezo hayo MKuu wa Wilaya ya Mkalama Moses Machali aliiomba CCM kuishauri Serikali izuie uingizwaji wa mafuta ya kula kutoka nje ya nchi ili kuyapa thamani mafuta ya alizeti yanayozalishwa nchini kwani hatua hiyo itasaiddia hatua mkulima wa ndani kunufaik na zao hilo
Machali amesema Uzalishaji wa alizeti umeongeza ndani ya Wilaya hiyo lakini changamoto kubwa ni bei ndogo , hivyo ni vema CCM na Serikali wakaona namna ya kusaidia kupandisha thamani ya zao hiloPicha mbalimbali za mkutano wa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo alipozungumza na wakazi na wanachama wa CCM Shina namba 5, Tawi la Iguguno Kaskazini, kata ya Iguguno wilaya ya Mkalama
Katibu Mkuu yupo kwenye ziara mkoani Singida yenye lengo la kukagua, kuhamasisha, kuhimiza na kusimamia Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025.
Katika ziara hiyo Katibu Mkuu ameongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Sophia Mjema pamoja na Katibu wa NEC Oganaizesheni Ndugu Issa Haji Ussi.