Wawakilishi pekee wa Kombe la Shirikisho Afrika timu ya Yanga SC imetoshana nguvu kwa kutoka sare ya bao 1-1 na timu ya Real Bamako ya nchini Mali katika mchezo uliochezwa leo Februari 26, 2023 nchini Mali.
Timu ya Yanga ndio iliyokuwa ya kwanza kupata bao la uongozi likipachikwa kambani na mshambuliaji wake Fiston Mayele katika dakika ya 60 ya kipindi cha pili cha mchezo huo.
Timu ya Yanga ilifanya mabadiliko ikiimarisha ulinzi kulinda goli lao ambapo zikiwa zimeongezwa dakika 4 kumalizika kwa mchezo huo, timu ya Real Bamako ilisawazisha goli hilo katika dakika ya 93 goli likifungwa na Emily Corne akipiga kichwa kuunganisha mpira wa kona uliomshinda mlinda mlango wa Yanga Didier Diara.
kufuatia mchezo huo timu ya yanga inashika nafasi ya pili katika kundi lao ikiwa na alama 4 nyuma ya RS Berkane ya Tunisia, ikifuatiwa na TP Mazembe yenye alama 3, na RS De Bamako ikishika mkia kwa kuwa na alama 2.