Home LOCAL WANAFUNZI SHULE YA SEKONDARI MAKITA HALMASHAURI YA MJI MBINGA,WAMSHUKURU RAIS SAMIA KUWAJENGEA...

WANAFUNZI SHULE YA SEKONDARI MAKITA HALMASHAURI YA MJI MBINGA,WAMSHUKURU RAIS SAMIA KUWAJENGEA VYUMBA VIPYA VYA MADARASA,WAHAIDI KUVITUMIA KUSOMA KWA BIDII

Na: Muhidin Amri, Mbinga

WANAFUNZI wa shule ya Sekondari Makita Halmashauri ya mji Mbinga mkoani Ruvuma,wameishukuru serikali kuwajengea vyumba vipya vya madarasa na kupunguza msongamano  mkubwa wa wanafunzi madarasani hivyo kuwasaidia kusoma katika mazingira mazuri.

Wamesema,wamefurahishwa na mpango wa serikali ya awamu ya sita kutokana na mkakati wake wa kuboresha na kuweka mazingira mazuri ya kujifunzia kwa wanafunzi na walimu kufundishia ikiwamo vyumba vipya vya madarasa,meza,viti na ofisi za walimu.

Pius Komba  mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika shule hiyo amesema,kutokana na uwekezaji huo wa serikali watahakikisha wanasoma kwa bidii na kufanya vyema katika masomo yao na hatimaye waweze kutimiza malengo yaliyowaleta shuleni.

Komba,amewaomba wazazi ambao  bado hawajapeleka watoto wao shule,kuhakikisha wanawapeleka haraka ili wakapate haki yao ya elimu kwani muda wa masomo umeshaanza na wao wamebaki nyumbani.

Aidha,amemshukuru Mkuu wa shule hiyo Mwalimu Emanuel Mwamasika kwa kukubali kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza hata wale wasiokuwa na mahitaji muhimu jambo linalowapa hamasa ya kusoma kwa bidii.

Happy Kinyunyu amesema,madarasa mapya yaliyojengwa kwa ubora yanawafanya wanafunzi  kupenda shule,kusoma kwa bidii na kuwa wasikivu darasani ikilinganishwa  na hapo awali kwa kuwa hakuna changamoto  zinazoweza kuwakatisha tamaa.

Amewaasa wanafunzi wenzake wa kike,kusoma kwa bidii ili kutimiza malengo yao badala ya kujiingiza katika ulevi,uesharati na kufanya kazi za nyumbani(House Girls) tabia iliyopelekea  baadhi ya watoto wa kike kushindwa kutumiza malengo yao.

Kwa upande wake Mkuu wa shule hiyo Emanuel Mwamasika amesema,walipokea kiasi cha Sh.milioni 40 ambazo zimefanikisha kujenga vyumba vipya viwili vya madarasa.

Amesema hapo awali kulikuwa  na uhaba mkubwa wa madarasa,lakini baada ya kupata fedha hizo na kujenga vyumba vipya sasa wanafunzi wanakaa  madarasani kwa nafasi na hakuna aliyekosa meza na kiti na wana ziada ya chumba kimoja.

Mwamasika,ameipongeza serikali ya Chama cha Mapinduzi kwa kutekeleza kwa vitendo Ilani yake jambo lililosaidia kuwa na mazingira mazuri na rafiki katika sekta ya elimu hapa nchini.

Mwamasika amesema,shule hiyo imepangiwa kupokea wanafunzi 332 wa kidato cha kwanza na hadi kufikia tarehe 4 wiki iliyopita wanafunzi walioripoti ni 220 sawa na asilimia 96.4.
MWISHO.

Previous articleTANZANIA, EU KUENDELEA KUSHIRIKIANA KATIKA UTEKELEZAJI WA MIRADI, KUIMARISHA UHUSIANO WA KIBIASHARA
Next articleTEF YAMUANGUKIA RAIS SAMIA MCHAKATO WA SHERIA YA HUDUMA ZA HABARI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here