Kaimu Msimamizi wa Huduma Ndogo za fedha (BoT), Bi. Mary Ngasa akisisitiza jambo alipokuwa akijibu maswali ya wahariri wa vyombo vya habari katika Mkutano wa Wahariri hao na BoT uliofanyika leo Februari 27,2023 Jijini Dar es Salaam.
Meneja Msaidizi Sera ya Fedha (BoT) Asimwe Bashagi akizungumza alipokuwa akitoa mada ya majukumu ya msingi ya Benki hiyo katika mkutano huo.
 Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Neville Meena akizumza kutoa neno la shukrani kwa niaba ya Makamu Mwenyekiti wa Jukwaa hilo wakati wa kuhitimisha kikao hicho.
Meneja Msaidizi Idara ya Mawasiliano Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Bi. Noves Moses (kushoto) akizungumza alipokuwa akihitimisha mkutano huo. (kulia) ni, Afisa Uhusiano Mkuu Mwandamizi wa Benki hiyo Lwaga Mwambande.
(PICHA ZOTE NA: HUGHES DUGILO)
Na: Hughes Dugilo, DAR.Â
Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imewaasa wananchi wanaotumia huduma ndogo za Fedha (Microfinance) kuacha kukopa fedha kwenye taasisi zisizosajiliwa na Benki hiyo.
Hayo yamesema na Kaimu Msimamizi wa Huduma Ndogo za fedha (BoT), Mary Ngasa wakati akijibu maswali ya wahariri wa vyombo vya habari mara baada ya kumaliza kuwasiisha mada ya Usimamizi wa Huduma Ndogo za Fedha, (Microfinance Supervision) katika Mkutano uliowakutanisha wahariri hao na BoT uliofanyika leo Februari 27,2023 kwenye ukumbi wa Benki hiyo Jijini Dar es Salaam.
Amesema kuwa Benki hiyo tayari imeshatoa mwongozo kwa watoa huduma ndogo za fedha kufanya usajili wa huduma hiyo kwani imeweka kiasi cha asilimia 3.5 kwa mwezi kama kiasi cha riba kwa mtoa huduma ndogo ndogo za mikopo ya fedha (microfinance).
“Ni kwa mujibu wa Benki Kuu (BoT) anayetoza riba zaidi ni mhalifu na anapaswa kuchukuliwa hatua za Kisheria”,amesema na kuongeza
“Tunawaomba wananchi kuzingatia usalama wa taasisi hizi wanazokwenda kukopa, msikope kwa mtu asiye na leseni ya BoT, na msikubali kukopa bila ya kujua masharti ya mkopo hususani suala la riba kuepusha kuzidishiwa makato,” amesisitiza Mary.
Aidha amewataka watoa huduma ndogo za Fedha (Microfinance) kujisajili katika Halmashauri zao ili waweze kupatiwa leseni za kutoa huduma hiyo kwani kutofanya hivyo watachukuliwa hatua za kisheria .