Home LOCAL WAGANGA WAKUU WALALAMIKIA UBOVU WA CHF, DKT MOLLEL ATOA MAJIBU

WAGANGA WAKUU WALALAMIKIA UBOVU WA CHF, DKT MOLLEL ATOA MAJIBU

Na:  WAF – DODOMA

Waganga Wakuu wa Mikoa (RMOs) na Halmashauri wameulalamikia ubovu wa Mfuko wa Afya Ngazi ya Jamii (CHF) kutokana na kutokukidhi mahitaji ya wananchi kupata huduma za afya katika maeneo mbalimbali nchini.

Hayo yamesemwa leo na Mwenyekiti wa RMOs Dkt. Best Magoma wakati akiwasilisa risala yake kwa Naibu Waziri wa Afya Dkt. Mollel (Mb) ambaye alikua mgeni rasmi katika mkutano wa RMOs uliofanyika leo jijini Dodoma.

Akijibu risala hiyo, Dkt. Mollel amesema ni kweli kumekua na malalamiko makubwa ya wananchi kutokupata huduma zinazokidhi viwango kupitia kadi za CHF.

“Kila ninapofanya ziara kwenye
Mikoa na Wilaya napokea malalamiko juu ya madhaifu makubwa ya CHF na wananchi wanadhani ndio kadi za Bima ya Afya ya Taifa ya (NHIF)” amesema, Dkt. Mollel.

“Nakiri kuwa CHF ni tatizo kila mahali hata huko nilikofanya ziara wananchi wanalalamikia CHF na wengi wanasema BIMA YA AFYA ukiwambia leteni kadi zenu wanaleta za CHF ambazo siyo NHF” amesisitiza Dkt. Mollel.

Dkt. Mollel amesema njia muafaka ya kuondokana na kero na malalamiko ya wananchi kwenye upatikanaji wa huduma ni kupitia muswada wa sheria ya bima ya afya kwa wote utaotoa nafasi kwa wananchi kupata huduma bora katika Hospitali zote nchini kuanzia Zahanati mpaka Hospitali ya Taifa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here