Home Uncategorized RC GEITA AIONGEZA RUWASA UCHAPAJI KAZI.

RC GEITA AIONGEZA RUWASA UCHAPAJI KAZI.

Mkuu wa Mkoa wa Geita Martine Shigela amewapongeza Wakala wa Maji na usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Mkoa wa Geita kwa utekelezaji bora wa miradi mbalimbali ya maji katika Mkoa huo.

Shigela amesema hayo katika kikao cha wafanyakazi wa RUWASA Mkoa wa Geita kilichofanyika katika ukumbi wa otonde mkoani humo amesema tangu kuanzishwa kwa mamlaka hiyo utekelezaji wa miradi ya maji umeimalika zaidi.

Amesema uwepo wa Mamlaka hiyo umesaidia kupunguza tatizo la ubadhilifu wa miradi ya maji hasa katika halmashauri uliokuwa ukijitokeza hapo awali na kusababisha miradi mingi kutokamilika kwa wakati na kusababisha wananchu kukosa huduma ya maji safi na salama kwani kwa sasa wananchi vijijini wanapata huduma hiyo kwa urahisi zaidi.

Amewataka wafanyakazi wa RUWASA mkoa wa Geita kutumia vyema kikao hicho kujadili mikakati mbalimbali itakayowezesha kuongeza kasi ya utendaji kazi ili kuongeza zaidi wigo wa upatiakanaji wa maji Vijijini.

Meneja wa RUWASA Mkoa wa Geita Mhandisi Jabiri Kayilla amempongeza Mhe Shigela kwa kufika katika kikao hicho huku akisema lengo la kikao hicho ni kujifanyia tathimini juu ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maji katika mkoa huo pamoja na wafanyakazi wa Mamlaka hiyo.

Mhandisi Jabiri kupitia kikao hicho amemuahidi Mkuu wa Mkoa wa Geita kuendele kusimamia vyema miradi mbalimbali ya maji Katika mkoa huo ili kufikia adhima ya serikali ya Kumtua mama ndoo kichwani.

Amesema mpaka sasa hali ya upatikanaji safi na salama imeimalika pakubwa katika Mkoa wa Geita amewataka mameneja wa RUWASA wilaya pamoja na wafanyakazi mbalimbali wa mamlaka hiyo kuongeza kasi zaidi ya utendaji kazi zaidi ili kufikia adhima ya serikali.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here