Home BUSINESS AFCFTA KIOO KUWA MIONGONI MWA BIDHAA ZITAKAZOTANGULIA AFCTA

AFCFTA KIOO KUWA MIONGONI MWA BIDHAA ZITAKAZOTANGULIA AFCTA

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.) akiangalia chupa iliyotengenezwa na Kiwanda cha Kioo Limited alipotembelea kiwanda hicho kuangalia bidhaa hiyo itakayoingizwa katika Soko la Eneo Huru la Biashara Barani Afrika (AfCFTA).

Mkurugenzi wa Kiwanda hicho Bwana Kumar Krishnan akimuelezea Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji jinsi chupa zinavyotengenezwa katika Kiwanda cha Kioo Limited alipotembelea kiwanda hicho kuangalia bidhaa hiyo itakayoingizwa katika Soko la Eneo Huru la Biashara Barani Afrika (AfCFTA).

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.)amekishauri Kiwanda cha Kioo Limited kuendelea kuzalisha bidhaa za kioo kwa wingi na zenye ubora na viwango vinavyohitajika kwa ajili ya Soko la Eneo Huru la Biashara Barani Afrika (AfCFTA).

Aidha, amekishauri Kiwanda hicho kuzalisha bidhaa za kioo zitakazotumika kama vifungashio kwa ajili ya wajasiliamali wadogo wadogo ili waweze kuhimili ushindani katika biashara na kuweza kuingia katika soko la AfCFTA.

Dkt. Kijaji ameyasema hayo alipotembelea Kiwanda cha Kioo Limied kilichopo Chang’ombe, jijini Dar es Salaam 14/02/2025 kwa lengo ya kuangalia bidhaa za kioo zinazozalishwa na kiwanda hicho zinazotarajiwa kuingizwa katika soko la AfCFTA.

Aidha, amesema Tanzania ni miongoni mwa nchi nane za mwanzo zilizopewa kipaumbele cha kupeleka bidhaa kwenye soko hilo ambapo miongoni mwa bidhaa 10 zitakazotangulia kuingia katika soko hilo kuanzia Julai Mosi 2023 ni pamoja na Kahawa, Marumaru na Kioo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kiwanda hicho Bwana Kumar Krishnan amesema Kiwanda cha Kioo kiko tayali kuingiza bidhaa ya kioo katika soko la AfCFTA kwa kuwa kiwanda hicho kinauwezo wa kizalisha zaidi ya chupa milioni moja (1) kwa siku ambazo huuzwa ndani na nje ya nchi.

Aidha ameeleza kuwa kiwanda hicho kinatengeneza kioo kwa kitumia malighafi zinazopatikana nchini kama mchanga, chokaa, felsper na magadi soda kutoka nje ya nchi kwa sasa.

Pia, amesema 40% ya chupa hizo hutengwnezwa na mabaki ya chupa zilizotumika hivyo amewaomba wanachi kukusanya kwa wingi mabaki ya chupa zilizotumika ili kurahisisha upatikanaji wa malighafi ya uzalishaji wa chupa hizo na kutunza mazingira.

Naye, Meneja wa Utawala Bwana Kapil Dave amesema kampuni hiyo iko tayali kuunga mkono juhudi zozote zinazofanywa na Serikali ikiwemo utekelezaji wa Mkataba wa AfCFTA

Previous articleMSIPANDISHE BEI ZA BIDHAA WAKATI WA MFUNGO WA RAMADAN NA KWARESMA: DKT. KIJAJI
Next articleDT. TAX AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA MKUTANO WA 42 WA BARAZA LA MAWAZIRI WA UMOJA WA AFRIKA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here