Home BUSINESS TANZANIA NA CHINA KUENDELEZA UHUSIANO WA KIBIASHARA 

TANZANIA NA CHINA KUENDELEZA UHUSIANO WA KIBIASHARA 

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya watu wa China zimeahidi kuendeleza uhusiano wa kibiashara baina ya nchi hizo kwa kuzingatia misingi ya uhusiano na ushirikiano wa kirafiki uliokuwepo tangu mwaka 1961 ili kuenzi mazuri yaliyofanywa na waasisi wa nchi zote mbili walioanzisha uhusiano huo.

Hayo yalisemwa na Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa China nchini, Mhe. Chen Mingjian katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam Februari 23, 2023

Dkt. Kijaji alisema Tanzania iko tayali kuendeleza uhusiano huo ili kuwawezesha wafanyabiashara wa pande zote mbili kushirikiana na kufanya biashara zao ili kuongeza ajira na kukuza uchumi wa wananchi na taifa kwa ujumla.

Aidha, Waziri Kijaji pamoja na Balozi huyo walijadiliana kuhusu namna ya kuenzi reli ya TAZARA na kufufua Kiwanda cha Urafiki ambacho ni matunda ya uhusiano baina ya nchi hizo pamoja na mikakati mbalimbali ya kuendeleza biashara.

Naye Balozi wa China nchini, Mhe. Mingjian amesema kuwa Serikali yake wakati wote imekuwa rafiki mzuri kwa Serikali ya Tanzania na uhusiano wa kibiashara ni mzuri na kwa sasa China inapokea parachichi ya Tanzania na iko tayari kupokea mazao mengine hususani maharage ya soya

Previous articleSERIKALI KUTANGAZA UTALII KUPITIA MBIO ZA KILIMANJARO
Next articleYASEMAVYO MAGAZETI JUMATATU YA LEO FEBRUARI 27-2023
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here