Home BUSINESS TFRA YAMFUTIA LESENI ALIYECHAKACHUA MBOLEA YA RUZUKU NJOMBE

TFRA YAMFUTIA LESENI ALIYECHAKACHUA MBOLEA YA RUZUKU NJOMBE

 

.
Mamlaka ya udhibiti wa mbolea Tanzania (TFRA) imemfutia leseni ya biashara wakala wa pembejeo anayedaiwa kuchakachua mbolea na kuwauzia wakulima mkoani Njombe hali iliyopelekea kuleta madhara makubwa ikiwemo kukauka kwa mazao ya baadhi ya wakulima shambani.
Mkurugenzi mtendaji mamlaka ya udhibiti wa mbolea Tanzania (TFRA) Dkt.Stephan Ngailo amebainisho hayo baada ya kufika mkoani humo na kukagua vidhibiti mbali mbali vilivyokamatwa na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa.
“Huyu amefanya udanganyifu,ubadhilifu na uhujumu uchumi hakuwa na nia njema na wakulima Kwa hiyo katika hatua ya kwanza tumeshamfutia leseni,huyu sio mfanyabiashara wa mbolea tena”Amesema Ngailo
Ngailo pia ameagiza zoezi la kutafuta wafanyabiashara wabadhilifu liweze kufanyika katika mikoa yote nchini hasa mikoa ya nyanda za juu kisini ili kudhibiti vitendo hivyo huku akiagiza kufidiwa wananchi waliopata hasara ya kununua mbolea bandia.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe Hamis Issah amesema tayari mpaka sasa watu zaidi ya 10 wakiwemo wanafamilia waliokuwa wanahusika kuchakachua mbolea wakitumia majengo na vifaa mbali mbali ikiwemo mifuko ya mbolea zaidi ya elfu kumi iliyokamatwa kwenye jengo chakavu lililopo mtaa wa Ramadhani mjini Njombe wamekwishakamatwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here