Home BUSINESS TANI 13 ZA SIGARA BANDIA ZATEKETEZWA GEITA.

TANI 13 ZA SIGARA BANDIA ZATEKETEZWA GEITA.

Na: Costantine James, Geita.

Kikosi cha kuzuia na kupambana magendo Kanda ya ziwa kimefanikiwa kukamata shehena ya sigara bandia tani 13.25 mkoani shinyanga zilizokuwa zinaingizwa nchini kinyume na sheria ambazo zingesababisha madhara ya kiafya kwa Watanzania takilibani milioni 11.

Akizungumza wakati wa zoezi la kuteketeza singara hizo bandia zilizoteketezwa katika kichomea taka kilichopo kwenye Mgodi wa GGML Mkoani Geita Meneja Msaidizi Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) Forodha Mkoa wa Mwanza Oswald Massawe amesema Shehena hiyo ya sigara za Magendo ilikamatwa Septemba 7, 2022 katika eneo la Luhumbi katikati ya Tinde na Isaka mkoani Shinyanga ikiwa inaingizwa nchini kwenye Loli lenye namba za usajiri T220 DCQ na tela lake namba T897 BVF.

Amesema loli hilo walilikamata likiwa mtu mmoja ambaye ni dereva peke yake jina lake halijatajwa alidai kabeba kahawa lakini baada ya uchunguzi walibaini kabeba Sigara ambazo ni bandia zenye thamani ya milioni 573.54 zikiwa zinaingizwa ichini kwa ajili ya matumizi ya binadamu kinyume na sheria ambapo mpaka sasa wanamshikilia huku mwenye mzigo huo mpaka sasa hajapatikana.

Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Shinyanga Faustine Cosmas amesema kwa kushirikiana na Mamlaka mbalimbali hapa nchini wameamua kuteketeza Bidhaa hizo baada ya kujilidhisha kuwa ni Sigara bandia na hazifai kwa matumizi ya binadamu.

Meneja wa Mamalaka ya Dawa na vifaa tiba (TMDA) Kanda ya ziwa Magharibi Geita Dkt. Edgar Mahundi amesema TMDA imejiridhisha sigara hizo hazifai kwani zingetumika zimekuwa chanzo kikubwa cha magojwa mbalimbali ikiwemo kansa kwa watumiaji.

Kwa upande wake Mkaguzi wa viwango kutoka Shirika la viwango Tanzania TBS amesema baada ya zigara hizo kukamatwa na TRA wao kama shirikika la viwango Tanzania walizipima na kugundua hazina Kiwango sitahiki na wamezikuta zikiwa haizina nembo ya shirika hilo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here