Home Uncategorized SIMBA SC YATEMBEZA ‘BOLI’ KWA MKAPA, YAICHAPA COASTAL UNION 1-0

SIMBA SC YATEMBEZA ‘BOLI’ KWA MKAPA, YAICHAPA COASTAL UNION 1-0

Timu ya mitaa ya msimbazi ya Jijini Dar es Salaam Simba SC imefaniwa kutinga hatua ya 16 ya michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam kwa kuichapa timu ya Coastal Union ya Tanga bao 1-0 katika Dimba la Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Goli la wekundu wa msimbazi lilipachikwa kambani na kiungo mkabaji wa timu hiyo Sadio Kanote katika dakika ya 56 ya kipindi cha pili ya mchezo huo kwa mkwaju mkali akipokea pasi kutoka kwa Pape Osman Sakho uliomshinda mlinda mlango wa Coastal Union.

Kufuatia kufuzu hatua hiyo timu ya Simba sasa inakwenda kucheza hatua inayofuata ya 16 bora ya mashindano hayo ambapo itacheza na timu ya African Spots wana ‘Kimanumanu’ ya Jijini Tanga.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Kocha wa timu ya Coastal Union Joseph Lazaro amesema matokeo hayo si mazuri kwao na kwamba wametumia mchezo huo kusoma mapungufu yaliyopo kwenye kikosi Chao na kwenda kufanya maboresho yatakayopelekea kufanya vizuri katika michezo ya Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara.

Previous articleWAZIRI MKUU MAJALIWA AKIZUNGUMZA NA DKT JINGU
Next articleWAMUOMBA RAIS SAMIA KUINGILIA KATI ILI HAKI ITENDEKE
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here