Home LOCAL RAIS DKT. SAMIA AFANYA UTEUZI WA VIONGOZI NANE

RAIS DKT. SAMIA AFANYA UTEUZI WA VIONGOZI NANE

 

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali.

Kupitia taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa mawasiliano ya Rais ikulu Zuhura Yunus Januari 16, 2023 imeeleza kuwa Rais Dkt.Samia amemteua Prof. Ahmed Mohamed Ame kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA).

Prof. Ame anachukua nafasi ya Mhandisi John S. Nduguru. Prof. Ame ni Mhadhiri, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Rais Dkt.Samia amemteua Bw. Eliud Betri Sanga kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Airtel Tanzania. Bw. Sanga anachukua nafasi ya Gabriel Malata aliyeteuliwa kuwa Jaji.

Bw. Sanga ni Mkurugenzi wa zamani wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSF).

Pia Rais Dkt.Samia amemteua Jaji (Mstaafu) Mathew Pauwa Mhina Mwaimu kuwa Mwenyekiti na Bw. Mohamed Khamis Hamadi kuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kwa kipindi cha pili.

Aidha, Rais Samia amewateua Makamishna wa Tume kama ifuatavyo:-

>Bw. Thomas Paulo Masanja, kuwa Kamishna wa Haki za Binadamu na Utawala Bora.

>Bi. Amina Talib Ali, kuwa Kamishna wa Haki za Binadamu na Utawala Bora.

>Bw. Khatibu Mwinyi Khatibu, kuwa Kamishna wa Haki za Binadamu na Utawala Bora.

>Bw. Nyanda Josiah Shughuli, kuwa Kamishna wa Haki za Binadamu na Utawala Bora.Kwa mujibu wa taarifa hiyo, utuezi huu ni kuanzia tarehe 15 Januari, 2023.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here