Home LOCAL CHAMA CHA MAPINDUZI ILALA WAJIPANGA KWA MIKUTANO

CHAMA CHA MAPINDUZI ILALA WAJIPANGA KWA MIKUTANO

 Na: Heri Shaaban (CCM ILALA)

Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Ilala kinajipanga kufanya Mikutano ya hadhara ya chama na ya Serikali katika Wilaya ya Ilala

Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi Wilaya ya Ilala Said Sidde , wakati wa kikao Maalum cha Halmashauri kuu Wilaya kwa ajili ya tamko la kufungua pazia mikutano ambapo alisema ndani ya Wilaya ya Ilala sasa kujipanga kwa ajili ya Mikutano ya chama na Serikali .

“Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ametoa ruhusa vyama vyote kufanya Mikutano ya hadhara nawaomba Wenyeviti wa Serikali za Mitaa mueleze Ilani ya Utekelezaji katika mikutano ya Serikali kazi zinazofanywa na Rais wetu sambamba na chama mjipange kila kata mfanye Mikutano Ikiwemo ya Jimbo “alisema Sidde .

Mwenyekiti Sidde alisema serikali yetu imefanya mambo makubwa katika nchi yetu Wilaya yetu na kata kuna maeneo Wenyeviti wa Serikali za Mitaa bado kufanya Mikutano naomba waanze vikao mara moja kuielezea Serikali kazi walizofanya .

Katika kikao hicho cha Halmashauri Kuu Wilaya pia walialikwa Viongozi wa Serikali wa Wilaya na Halmashauri ya Jiji kwa ajili ya kusikiliza changamoto Ili ziweze kufanyiwa kazi CCM Ilala na Serikali wanafanya kazi pamoja

Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Omary Kimbilamoto alisema HALMASHAURI hiyo inampongeza Mwenyekiti wa CCM WIlaya ya Ilala kwa kufanya kazi vizuri na Serikali pamoja na Chama Mwenyekiti wa CCM anaupiga mwingi ameshafanya vikao na Watendaji wa Halmashauri pamoja na Wenyeviti wa Serikali za Mitaa pamoja na madiwani kwa Dhumuni la kujenga Wilaya Ilala .

Meya Kumbilamoto alisema Mikutano itakapoanza waende kuelezea utekelezaji wa Ilani unaofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, ambaye ameleta fedha nyingi za maendeleo za miradi mikubwa ya Afya ,miundombinu ya Barabara na sekta ya Elimu ambapo Ilala inajenga madarasa 310.

Aidha alisema pia Serikali imejenga madaraja ya kisasa Ulongoni GONGOLAMBOTO madaraja mawili yanaunganisha na Kinyerezi pamoja na shule ya kisasa English Medium iliyopo GONGOLAMBOTO ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya Serikali ya awamu ya sita na Sasa wanajenga uwanja Michezo wa Kisasa GONGOLAMBOTO na sehemu ya Bustani ya kupumzukia Wananchi wa Ilala Mnazi Mmoja .

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji Amani Mafuru alisema amepokea kero za Kata 36 za Wilaya ya Ilala anaenda kuzifanyia kazi zikiwemo kero za miundombuinu na kero kubwa Tano .

Amani Mafuru alisema akizungumzia Miundombinu ya Barabara kuna pesa za TANRODS Wana Barabara zao za mkoa na TARURA Barabara Unganishi ila kwa Sasa BARABARA za TARURA wakitangazwa zinafanyiwa usanifu ndio zinajengwa .

Mwisho

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here