Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Prof. Elisante Ole Gabriel akizungumza alipokuwaakitoa mada katika Mkutano wa viongozi waandamizi wa Mahakama ya Tanzania na Wahariri wa vyombo vya habari uliofanyika leo Disemba 16,2022 katika kituo Jumuishi cha utoaji Haki Jijini Far es Salaam.
Msajili wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Sylvester Kainda akitoa mada kuhusu uendeshaji wa mashauri katika mahakama katika Mkutano huo.
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Prof. Elisante Ole Gabriel (kushoto), akiwa na Mkuu wa kitengo cha Maboresho Mahakama ya Tanzania Dkt. Angelo Rusha (kulia) wakifuatilia mada iliyokuwa ikiwasilishwa na Msajili wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Sylvester Kainda
Badhi ya Wahariri wa habari wakifuatilia Mkutano huo
Mkuu wa kitengo cha Maboresho Mahakama ya TanzaniaĀ Dkt. Angelo Rumisha akiwasilisha mada kwenye Mkutano huo.
PICHA NA: HUGHES DUGILO.
Na: Mwandishi wetu, DSM
VIONGOZI waandamizi wa Mahakama ya Tanzania wamekutana na wahariri wa vyombo mbalimbali nchini wakiongozwa na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania(TEF) Deodatus Balile huku Mahakama hiyo ikitumia nafasi hiyo kuelezea maboresho yaliyofanyika ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za kimahakama kwa Watanzania.
Pamoja na mambo mengine viongozi wa Mahakama ya Tanzania wameelezea ujenzi wa miundombinu ya jengo la kisasa la Mahakama ambalo lina ukubwa wa squre mita 60000, na litakuwa la sita kwa ukubwa duniani.Jengo hilo ujenzi wake unatarajia kukamilika mwishoni mwa Desemba mwaka 2022, Mjini Dodoma.
Akizungumza mbele ya wahariri hao, Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Profesa Elisante Ole Gabriel amesema wana malengo matatu ya kukutana na wahariri, limegawanyika katika sehemu tatu, kwanza ni kuendelea kuimarisha uhusiano kati ya Mhimili wa Mahakama na vyombo vya habari, na ili lifanikiwe linahitaji wahariri kwasababu waandishi wa habari siku zote wanapeleka taarifaa kwa wahariri.
āJambo la msingi ni kuhakikisha wahariri na waandishi wanaelewa jinsi maboresho yanavyofanyika ndani ya Mahakama , ni mambo gani yamefanyika toka kipindi cha Uhuru hadi sasa.Pia matumizi ya TEHAMA yalivyobadilika, matumizi ya kifikra na mambo mengine kama hayo na tuliamini kuna haja ya kupata wahariri, kusudi ile tasnia ya habari iweze kuelewa kinagaubaga kinachoendelea.
āLakini jambo la tatu na la msingi wahariri na waandishi wa habari watusaidie kuelimisha na kuhabarisha umma wa Watanzania, ili wananchi wafahamu katika kila haki wanayostahili kupata wana wajibu wao , hawa wananchi wanawajibu wa kufanya katika kuhakikisha haki yao inatendeka kwa wakati,āamesema .
Amefafanua, kwa mfano suala la ushahidi ni jukumu la anayetafuta haki yake , yeye ndiye anayejua haki ile ikoje huku akitumia nafasi hiyo kukiri wazi kuona wahariri wamekuwa na muamko mkubwa kuelewa yale ambayo wamekuwa wakiyazungumza.
āKwa mfano maboresho katika ufunguaji wa kesi, na hata muundo mzima wa Mahakama. Nitoe mwito wangu kwa Watanzania kuthamini na kuheshimu maboresho yaliyofanyika ndani ya Mahakama na Jaji Mkuu ambaye ndiye kiongozi wetu amekuwa anatueleza tufanye kila linalowezeakana huduma zetu ziwe na sifa kuu tatu, zitolewe kwa weledi, uwazi lakini pia kwa kuhakisha wanaokoa muda wa wananchi wakafanye shughuli nyingine za kiuchumi.
āLakini sambamba na hilo haya mabadiliko na maboresho yasingefanyika bila rasilimali fedha , tunaishukuru Serikali inayoongozwa na Dk.Samia Suluhu Hassan pamoja na wasaidizi wake hususani Wizara ya Fedha chini ya Waziri Dk.Mwigulu Nchemba na Katibu Mkuu Emaenul Tutuba kwa jinsia ambavyo tunahitaji rasilimali fedha kwa kweli wanatupatia kwa wakati ili kufanikisha haya maboresho.ā
Amesisitiza wanapohitaji rasilimali fedha wamekuwa wakipatiwa kwa wakati na kwamba wanatamani wananchi wazidi kupata huduama kwa haraka huku akieleza Mahakama ya sasa ni ya Kidigi.
Kuhusu kuhamia Dodoma , Profesa Gabriel amesema Serikali imeendelea kuwawezesha, hivyo jengo la Mahakama linaendelea vizuri na mpango wao uko pale pale watalipokea jengo mwishoni mwa Desemba ili taratibu nyingine za kuweka samani ziendelee.
āJengo lile litakuwa la sita kwa ukubwa duniani kwasababu litakuwa na ukubwa wa Squre mita 60,000 na niseme lina matawi matatu makubwa, moja ni la Mahakama Kuu, Mahakama ya Rufani na Mahakama ya Juu , na kutakuwa na jengo la utawala pale katikati.Watu wengi wanajiuliza kwenye Katiba kwamba Mahakama ya Juu haipo, ndio kusema tunawashukuru sana viongozi wetu wakati maboresho haya yanafanyika Balozi Hussein Katanga pamoja na Jaji Othman Chande.
āWalisema katika mchoro iwepo Mahakama ya Juu hata kama kwa sasa haijaanza kutumika ili itakapoanza tusiingie gharama za ujenzi, niseme tu wakati huo utakapofika kwa kuwa miundombinu ya majengo yatakuwepo kwa ajili ya Mahakama ya Juu hivyo Serikali itawezesha masuala ya rasilimali nyingine ikiwemo rasimali watu na vitendea kazi vingine ili kazi iendelee kwa wakati huo ambao Katiba itakuwa imeelekeza uwepo wa Mahakama ya Juu,āamesema.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania(TEF) Deodatus Balile ametumia nafasi hiyo kuishukuru Mahakama kwa kukutana na wahariri huku akitumia nafasi hiyo kuwapingeza kwa mageuzi makubwa yanayoshuhudiwa katika mifumo na miundombinu.
āWamekuwa na fikra chanya hata ile hofu kwamba labda ukibadilishwa mfumo basi watakosa kazi , hoja ya kubadilisha muundo ndani ya Mahakama watu wabadilike kama alikuwa Sekretari basi awe Hakimu au kama aende uraini awe Wakili, ni jambo linalotia moyo , nchi yetu inafikia mambo makubwa kama haya kwa kutumia watalaamu wetu wa ndani basi kumbe tukiunganisha hii minyororo kumbe shida sio rasilimali bali ni mawasiliano ndani ya taasisi.ā
Mwisho