Home Uncategorized TANZANIA, ZAMBIA WAKUTANA KUJADILI USALAMA BOMBA LA MAFUTA Na Beatrice SANGA- MAELEZO

TANZANIA, ZAMBIA WAKUTANA KUJADILI USALAMA BOMBA LA MAFUTA Na Beatrice SANGA- MAELEZO

Na:  Beatrice SANGA- MAELEZO

Waziri wa Nishati Mh. January Makamba amekutana na waziri wa nishati Zambia Mh. Peter Chibwe Kapata pamoja na viongozi wa Ulinzi na Usalama ili kujadiri namna ya kuongeza ulinzi na usalama wa Bomba la mafuta la Tanzania-Zambia Crude Oil Pipeline (tazama Pipeline) Mara baada ya kubadirisha matumizi kutoka kusafirisha mafuta ghafi hapo awali na sasa kusafirisha mafuta ya dizeli.

Akizungumza katika kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Hyatt Regency Jijini Dar es Salaam Mh. January Makamba ameeleza kuwa Mara baada ya serikali ya Zambia kubadirisha matumizi ya Bomba Hilo kutoka kusafirisha mafuta ghafi na sasa kusafirisha mafuta ya dizeli Bomba Hilo kwa sasa linahitaji ulinzi zaidi ili kulinda usafilishwaji wa mafuta hayo na ndo maana wamekutana viongozi wa pande zote mbili ili kujadili usalama wa Bomba Hilo.

“Kama mnavyofahamu Tanzania na Zambia Zina mradi wa muda mrefu ulionzishwa na Marais waanzilishi wa hizi nchi mbili, ambao ni Bomba la mafuta Kati ya nchi hizi mbili, huko nyuma Bomba la mafuta lilikuwa linasafirisha mafuta ghafi Sasa miaka kadhaa iliyopita serikali ya Zambia iliamua kubadirisha ili Bomba liache kisafirisha mafuta ghafi lisafilishe mafuta ya diseli na kutokana na hiyo ikafanyika manunuzi ya kuwezesha Bomba Hilo kubadirishwa na ni ya gharama kubwa, lakini ukishaanza kisafirisha diseli maana yake usalama wa Bomba na lenyewe unakuwa ni jambo kubwa kwa sababu mafuta Yale ghafi ni mafuta ambayo hata mtu akiyaiba njiani hayafanyi kazi yoyote lakini unaposafirisha dizeli hatari ya njiani mafuta kuchepushwa ni kubwa zaidi kwahiyo Sasa tukaamua serikali zetu mbili kufanya uratibu wa usalama wa hili Bomba” Amesema Mh. Makamba

Kwa upande wake waziri wa Nishati nchini Zambia Mh. Peter Chibwe Kapata ameeleza kuwa hapo awali ambapo walikuwa wanasafirisha mafuta ghafi kutoka Tanzania kwenda Zambia ambako yanachakatwa gharama za uendeshaji zilikuwa kubwa na serikali yao ilikuwa ikitumia ruzuku kubwa hivyo ni wakati sasa wamefanya mapinduzi kwa kusafirisha mafuta ambayo tayari yameshachakatwa ,lakini pia ni wakati wa kufikiria ikiwezekana waweze kujenga Bomba la kusafirisha gesi kutoka Tanzania kwenda Zambia hali itakayosaidia kupunguza ukataji miti ovyo kwa ajili ya mkaa na kuni na kuwezesha kutunza mazingira.

Naye Waziri wa ulinzi Zambia, Mhe. Ambrose Lufuma aameishukuru serikali ya Tanzania kwa kuwa mwenyeji wa jambo hili pamoja na timu ya ufundi kwa kufanya kazi nzuri ndani ya siku mbili walizo kaa ambapo wameweza kuja na mipango mbalimbali itakayotumika kulinda bomba Hilo ikiwemo ufungaji wa camera za CCTV, matumizi ya drones na kuweka askari kwa ajili ya ulinzi masaa yote

“Sote tunafahamu kuwa bomba lililopita lilikuwa linabeba mafuta machafu na mafuta ghafi ambayo yalikuwa hayavutii kama haya ya sasa ambayo yameshachakatwa hivyo tunahitaji kulilinda bomba hili na ndio maana tuko hapa kujaribu kuona jinsi tutakavyolilinda. Tumepokea mawazo mbalimbali na tunaendelea kuzungumza juu ya kuongeza ulinzi, ili kuweza kuweka usalama masaa ishirini na nne na pia tutaweka drones, na cctv hii yote ni kulitunza na kulilinda bomba hili.”Amesema Mhe. Lufuma.

Previous articleDKT.MOLLEL AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA MRATIBU WA MALARIA WA DUNIA DKT. DAVID WILTON
Next articlegiZ YAPONGEZA UBORA WA BIDHAA ZA WAJASIRIAMALI WA TWCC
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here