Home Uncategorized CCM WILAYA YA GEITA YACHANGIA TOFARI 250 UJENZI WA MADARASA MSETO SHULE...

CCM WILAYA YA GEITA YACHANGIA TOFARI 250 UJENZI WA MADARASA MSETO SHULE YA MSINGI

Chama cha Mapinduzi wilaya ya Geita kimeshiriki uchimbaji wa Msingi wa vyumba viwili vya Madarasa katika shule ya Msingi Mseto iliyopo kata ya Kalangalala Halmashauri ya mji wa Geita

Akizungumza Baada ya zoezi la kuchimba Msingi wa Madarasa hayo kwa Niaba ya Chama cha Mapinduzi katibu Siasa na Uenezi wa CCM wilaya ya Geita Ndg Gabriel Masunga Nyasilu (Gebo) alisema pamoja na Chama kuwa na jukumu la kuisimamia serikali katika kutekeleza ilani ya uchaguzi bado wanao wajibu wakushiriki moja kwa moja kwenye Shughuri za Maendeleo na kutoa wito kwa wanachi kuendelea kujitolea katika shughuri za Maendeleo ili kuunga Mkono juhudi za serikali ya awamu ya sita (6)

Katika kufanikisha zoezi hilo la ujenzi wa madarasa Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Geita na Diwani wa kata ya Mtakuja Mh *Costantine Morandi* ambaye pia ni Mkazi wa Mtaa huo amechangia Toafari 800 kwa ajiri ya ujenzi huo,,

Naye Mwenyekiti wa umoja wa vijana wa CCM Mkoa wa Geita ndug Manjale Nkilosubi Magambo amechangia Tofari 500 katika Zoezi hilo la ujenzi wa Madarasa kwenye shule hiyo ambayo yeye Binafsi amesomea hapo elimu ya Msingi,,

Katika zoezi hilo ambalo Mgeni Rasmi alikuwa Mkuu wa wilaya ya Geita aliyewakilishwa na Katibu Tarafa wa Tarafa ya Geita kupitia ofsi yake alichangia mifuko 22 ya saluji ili kuunga Mkono juhudi za wananchi kwenye ujenzi wa Madarasa hayo,,

Wadau wengine waliochangia Ujenzi huo wa Madarasa ni Mh Diwani wa kata ya Kalangalala , Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa lwenge ,, na wadau Mbalimbali wa Maendeleo ndani na nje ya Mtaa huo,,

Chama cha mapinduzi wilaya ya Geita kitaendelea kushirikiana na serikali, wananchi katika shughuri zote za maendeleo ndani ya wilaya yetu,,

Kidumu chama cha mapinduzi Imetolewa na Gabriel nyasilu Katibu Siasa na uenezi wilaya ya Geita

Previous articleBALOZI FATMA ASAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO UBALOZI MDOGO WA CHINA
Next articleARMED INTRUSION OF NORTH MARA RESULTS IN ONE CASUALTY
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here