Home LOCAL WABUNGE WAJENGEWA UELEWA KUHUSU DHANA YA BIMA YA AFYA KWA WOTE

WABUNGE WAJENGEWA UELEWA KUHUSU DHANA YA BIMA YA AFYA KWA WOTE

WAF, Dodoma

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema chimbuko la Muswada wa Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote ni kutimiza wajibu wa kikatiba wa kila mwananchi awe na uhakika wa matibabu pindi anapougua.

Kauli hiyo ameitoa leo tarehe 3 Novemba, 2022 wakati wa kuwajengea uelewa Wabunge wa Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania kwenye ukumbi wa Pius Msekwa jijini Dodoma.

Waziri Ummy amesema lengo la Sheria hiyo ni kuhakikisha kila Mtanzania anapata matibabu bila ya vikwazo vyovyote kwenye vituo vya kutolea huduma za afya nchini.

Aidha, Waziri Ummy amesema Wizara imekiwekea kipindi cha miezi sita ili kuweza kutoa elimu kwa umma kuhusu dhana nzima ya Bima ya afya kwa wote.

“Sote ni mashahidi tumeona wananchi wengi wanauza mashamba na mali zao ili kuweza kupata fedha za matibabu pindi wanapougua”.

Amesema kuwa na bima ya afya kwa wote itasaidia wannchi wote hata wale wasio kuwa na uwezo kuwa na uhakika wa matibabu wakati wowote.

Naye,Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya huduma na Maendeleo ya Jamii Mhe. Stanslaus Nyongo amesema Bima ya Afya kwa Wote itaenda kuwasaidia wananchi kwenye matibabu,pia suala hilo ni sehemu ya Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025.

Wakati huo huo Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. George Simbachawene amesema kutokana na mabadiliko ya mfumo wa maisha kumekuwa na changamoto za afya hivyo ni wakati muafaka wa kuwa na Bima ya Afya kwa Wote.

Previous articleWAZIRI UMMY APOKEA MASHINE 50 ZENYE UWEZO WA KUTIBU MABADILIKO YA AWALI YA SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI
Next articleBRELA YATOA MAFUNZO YA MILIKI UBUNIFU KWA WABUNGE
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here