Home BUSINESS SERIKALI YAWARAHISISHIA WAFANYABIASHARA UTOAJI RISITI ZA EFD

SERIKALI YAWARAHISISHIA WAFANYABIASHARA UTOAJI RISITI ZA EFD

Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb) akijibu swali bungeni jijini Dodoma.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WFM, Dodoma).Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) akiteta jambo na Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Mhe. George Simbachawene pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi, bungeni jijini Dodoma.Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Hamad Hassan Chande wakiteta jambo, bungeni jijini Dodoma.

Na. Haika Mamuya na Farida Ramadhani, WFM, Dodoma

Serikali kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imeanzisha mfumo rahisi wa utoaji wa risiti ujulikanao kama Visual Fiscal Devices (VFD) ili kuhakikisha kuwa kila mfanyabiashara anapata mashine za Kutolea Risiti za Kielektroniki (EFD) kwa njia rahisi na isiyo na gharama.

Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb) alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mhe. Subira Khamis Mgalu aliyetaka kujua mpango wa Serikali wa kugawa mashine za kutolea risiti EFD kwa Wafanyabiashara ili kuongeza wigo wa walipa kodi.

Mhe. Chande alisema kuwa Mfumo huu wa kisasa wa utoaji wa risiti hauhitaji kutumia mashine kama ilivyo sasa badala yake mtumiaji anaweza kutumia vifaa vingine vya kieletroniki kama vile simu janja, kompyuta na vishikwambi kutoa risiti zilizounganishwa na mfumo wa TRA.

“Mfumo unaendelea kutumika na kusambaa nchi nzima na hauna gharama badala yake mtumiaji ataingia gharama ndogo ya bando ili kupata mtandao wakati wa matumizi”, alifafanua Mhe. Chande.

Aidha, alisema kuwa wafanyabiashara wanaruhusiwa kisheria kujirejeshea gharama ya ununuzi wa mashine za EFD wakati wa uandaaji wa hesabu zao za kodi wanazopaswa kulipa.Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.

Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) akiteta jambo na Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Mhe. George Simbachawene pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Dkt. Eliezer Feleshi, bungeni jijini Dodoma.

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Hamad Hassan Chande wakiteta jambo, bungeni jijini Dodoma.Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb) akijibu swali bungeni jijini Dodoma.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here