Home BUSINESS BENKI YA LETSHEGO YASHIRIKI WIKI YA HUDUMA ZA KIFEDHA JIJINI MWANZA

BENKI YA LETSHEGO YASHIRIKI WIKI YA HUDUMA ZA KIFEDHA JIJINI MWANZA

Msimamizi wa Masoko, Mawasiliano na Huduma kwa Wateja wa Benki ya Letshego Selestino Nachenga (kushoto) akizungumza na wananchi waliotembelea katika Banda la Benki hiyo kwenye wiki ya Huduma za Fedha Jijini Mwanza. (katikati) ni, Farida Mhina Afisa Mahusiano wa Benki hilo Tawi la Mwanza, na (wa tatu kushoto) ni, Afisa Mahusiano kutoka Makao Makuu ya Benki hiyo Jijini Dar es Salaam Deric Deric.

Maafisa Mahusiano wa Benki   ya Letshego, Farida Mhina(wa kwanza kushoto)na Deric Deric (wa pili kushoto) wakitoa elimu kwa wananchi waliotembelea Banda la Benki hiyo katika Maonesho hayo.

Msimamizi wa Masoko, Mawasiliano na Huduma kwa Wateja wa Benki ya Letshego Selestino Nachenga (kushoto) akitoa zawadi kwa wananchi hao.

Bw. Ramadhan Ameir (kushoto) akipokea zawadi kutoka kwa Msimamizi wa Masoko, Mawasiliano na Huduma kwa Wateja Benki ya Letshego Selestino Nachenga (kulia) wakati mgeni huyo alipotembelea Banda la Benki hiyo kufahamu shughuli mbalimbali zinazofanywa na Taasisi hiyo.

2022.Benki ya Letshego Tanzania imeungana na kampuni na taasisi nyingine zinazojihusisha na utoaji wa huduma za kifedha Nchini Tanzania katika Maadhimisho ya wiki ya huduma za kifedha.

Kwa mwaka huu wa 2022 Monyesho haya yanafanyika Mkoani Mwanza katika viwanja vya Rockcity Mall.Katika kuunga mkono kaulimbiu ya wiki ya Huduma za kifedha kitaifa ya mwaka huu; Elimu ya Fedha kwa Maendeleo ya watu;

Benki ya Letshego inaendelea kuwekeza na kukuza biashara yake kwa kubadilisha utoaji bidhaa na huduma zake, kuweka njia za kidijitali ili kuongeza uzoefu wa wateja na vile vile kuwezesha upatikanaji rahisi wa suluhu za kifedha kwa bei nafuu kwa wateja wengi zaidi ikiendelea kutilia mkazo kwenye utoaji wa elimu ya kifedha kwa wateja wake kwenye kila huduma Inazozitoa.

Akizungumza na Mwandishi wetu, Bw. Omar Msangi, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Letshego alisema; “Benki ya Letshego ilizindua Mkopo Fasta – bidhaa iliyoundwa na Letshego ili kusaidia wafanyabiashara wadogo kuondokana na changamoto za mzunguko wa pesa. Mkopo Fasta huongeza upatikanaji wa mtaji, haraka na kwa urahisi, ili kuwezesha biashara ndogo kununua bidhaa, kukidhi gharama za biashara au hata kusaidia gharama zozote za uzalishaji zinazohitajika ili kukidhi mahitaji ya wateja kwa wakati.

Bwana Msangi aliongezea, “Mara maombi yakishaidhinishwa, fedha taslimu huwekwa kwenye akaunti za wafanyabiashara ndani ya saa 72, na hivyo kufungua fursa ya mapato na ukuaji wa uchumi.”

Mbali na kusaidia biashara ndogo ndogo, Benki ya Letshego pia inasaidia watu binafsi kwa kutoa masuluhisho ya kifedha na bidhaa kwa vijana, afya, ustawi, akiba na kustaafuPia Benki ya Letshego inakwambia kwa nini uteseke kulipa Bima kwa Mkupuo? LetsGo Bima Loan ni suluhisho.

Huu ni mkopo unaoteolewa na benki ya Letshego Tanzania kwa ajili ya Malipo ya Bima. Mkopo huu unakupa unafuu na nafasi ya kulipa Bima yako kidogo kidogo mpaka miezi 10.

Lakini Pia Bw. Omar Msangi katika utoaji wa huduma zote hizi Elimu ya fedha Kwa wateja wetu ni siuala la kipaumbele tukiendelea kuunga mkono jitihada za serikali katika masuala mazima ya utoaji wa elimu ya Fedha kwa Maendeleo ya watu.

Benki ya Letshego Tanzania ni mojawapo ya kampuni tanzu 11 za Afrika nzima ndani ya Letshego Holdings Group, yenye makao yake makuu na kuorodheshwa nchini Botswana. Kundi hili linalenga kuwawezesha wafanyabiashara wa Kiafrika katika hatua ndogo, ndogo na za kati, MSMEs na kuboresha maisha ya raia wa kawaida kupitia utoaji wa masuluhisho ya kibunifu ya kifedha.Kundi hili limezindua huduma yake inayojulikana kwa jina la Digital Mall, jukwaa la benki ya kidijitali ambapo wateja wanaweza kutuma maombi ya mikopo, bima, akaunti za akiba na bidhaa zingine za mtindo wa maisha.Benki ya Letshego (T) yenye makao yake makuu Morocco, Dar es Salaam, na ina mtandao wa ofisi tisa, mawakala, ATM , na ni sehemu ya mtandao wa ATM za Umoja Switch nchini Tanzania na mtandao wa ATM za VISA.

Previous articleWAGANGA WATOE DAWA KULINGANA NA MAJIBU YA MAABALA – PROF. NAGU
Next articleBOT, HAKIKISHA MNAWALINDA WATUMIAJI WA HUDUMA ZA FEDHA – DKT. MPANGO
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here