Home LOCAL ELIMU ZAIDI INAHITAJIKA KUEPUKA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA

ELIMU ZAIDI INAHITAJIKA KUEPUKA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA

Kaimu Meneja Mpango wa kudhibiti Magonjwa Yasiyoambukiza Bi. Valeria Milinga.

Katibu Tawala Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Jijini Mwanza Bw. Petro Sabato akielezea umuhimu wa utoaji wa elimu juu ya Magonjwa yasiyoambukiza katika siku ya kisukari Duniani ambapo kitaifa yamefanyika Jijini Mwanza.

Mwenyekiti wa Chama cha Kisukari Tanzania Prof. Andrew Swai.

Na. WAF – Mwanza

Watanzania wanahitaji elimu zaidi ili waweze kuepukana na magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo ugonjwa wa Kisukari ambao umekua ukiongezeka nchini.

Hayo yamesemwa leo na Katibu Tawala Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Bw. Petro Sabato kwenye madhimisho ya siku ya Kisukari Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika Wilaya ya Misungwi Jijini Mwanza.

“Elimu inahitajika zaidi ili kuwakinga wananchi na Magonjwa Yasiyoambukiza hasa Kisukari kwa kuwa ugonjwa wa Kisukari umekua ukigharimu maisha ya watu ikiwa ni pamoja na kukatwa baadhi ya viungo .” Amesema Bw. Sabato

Aidha, Bwa. Sabato ametoa rai kwa wananchi kufanya mazoezi sambamba na kupima Afya angalau mara moja kwa mwaka ili ukigundulika mapema inakuwa rahisi kupata matibabu.

Kwa upande wake Kaimu Meneja Mpango wa Kudhibiti Magonjwa Yasiyoambukiza Bi. Valeria Milinga amesema vifo vitokanavyo na magonjwa yasiyoambukiza yanachangia kwa asilimia 33 huku ugonjwa wa kisukari ukiwa ni 9.10%

“Katika kuongeza uhamasishaji na uelewa kwa wananchi juu ya magonjwa yasiyoambukiza hasa ugonjwa wa kisukari tumeweza kufanya maonyesho ya wiki ya magonjwa yasiyoambukiza yaliyoanza tarehe 5-12, Novemba 2022 ambayo yanafanyika kila mwaka.” Amesema Bi. Milinga

Aidha, Bi. Milinga ametaja mafanikio ya maonyesho hayo kwa mkoa wa Mwanza hadi kufikia siku ya kilele tarehe 12, Novemba, 2022 wananchi takriban 3000 wamejitokeza kupima ugonjwa wa Kisukari na 34 kati yao wamegundulika kuwa na ugonjwa huo.

Hatahivyo, amebainisha mafanikio waliyoyapata katika utoaji wa huduma za kisukari ikiwemo upatikanaji wa Dawa, utoaji wa mafunzo kwa watoa huduma za Afya katika Vituo 300 kwenye Mikoa 9.

Naye, Mwenyekiti wa Chama cha Kisukari Tanzania Prof. Andrew Swai amesema miaka ya 1991 kulikuwa na 1% tu ya ugonjwa wa kisukari nchini lakini kwa sasa imeongezeka hadi kufikia 9%.

“Kutokana na ongezeko la ugonjwa wa kisukari nchini imekua tatizo ambapo inagharimu 20% ya bajeti ya Serikali ili kuwahudumia wagonjwa hao.” Amesema Prof. Swai

Maadhimisho hayo yameandaliwa na Wizara ya Afya kwa kushirikiana na wadau wa Chama cha Kisukari Tanzania (TDA), Shirikisho la Vyama vya Magonjwa Yasiyoambukiza (TNCDA) na viongozi wa Mkoa wa Mwanza wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya.

#MtuNiAfya
#JaliAfyaYako

Previous articleKAMATI YA BUNGE YA ARDHI, MALIASILI NA UTALII YARIDHISHWA NA UBORESHWAJI WA MIUNDIOMBINU YA HIFADHI YA TAIFA KILIMANJARO
Next articleMAGAZETI YA LEO JUMATATU NOVEMBA 14-2022
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here