Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya ILALA Said Sidde akisaini kitabu cha Wageni katika Shirika la Sauti ya Jamii Kipunguni alimsindikiza Meya wa Halmashauri ya Jiji Omary Kumbilamoto katika Utekelezaji wa Ilani (aliyesimama)Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Kipunguni Daniel Malagashimba Leo Octoba 07/2022 (PICHA NA HERI SHAABAN)
Meya wa Halmashauri Jiji Omary Kumbilamoto (Katikati)akikabidhi Feni Shirika la Sauti ya Jamii Kipunguni mbele ya Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala Said Sidde Leo Octoba 07/2022 ,wengine Diwani wa Kata ya Kipunguni Steven Mushi,Mwenyekiti wa Mtaa Amani Daniel Malagashimba na Mkurugenzi wa SAUTI ya Jamii Seleman Bishagazi (PICHA NA HERI SHAABAN)
Na: Heri Shaaban (Ilala)
MEYA wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Omary Kumbilamoto, amempongeza Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Ilala Said Sidde aliyechaguliwa katika Uchaguzi Mkuu wa CCM Wilaya ya Ilala Octoba 2022 mwaka huu.
Meya Kumbilamoto alitoa pongezi hizo katika ziara yake ya kiserikali Kata ya Kipunguni Shirika la Sauti ya Jamii Kipunguni alipokwenda kukabidhi feni na Televisheni shirika hilo katika sehemu ya ahadi yake.
“Nakupongeza Al haj Said Sidde umeshinda kwa kishindo Uchaguzi Mkuu wa Wilaya ya Ilala Octoba mwaka huu,baada kuchaguliwa kushinda ulinita ofisini kwako nikaja ukataka nikueleze ahadi zote na kazi tunazofanya ufatilie zikiwemo za Madiwani na Viongozi wote wa Ilala “ alisema Kumbilamoto.
Meya Kumbilamoto alisema amekabidhi Televisheni na Feni sehemu ya ahadi yake katika Shirika la Sauti ya Jamii Kipunguni kwa ajili ya Shirika hilo .
Akizungumzia Kata ya Kipunguni Kumbilamoto alisema Serikali imetekeleza Ilani kwa vitendo katika kata hiyo sekta ya Elimu imejenga madarasa 18 na mikakati mingine kwa ajili ya shule ya gholofa .
Aidha Meya Kumbilamoto alisema pia serikali imejenga kituo Cha Afya Cha Serikali katika kata ya Kipunguni na Mikakati mingine kata Kipunguni Serikali INATARAJIA kujenga kituo Cha afya Eneo la Moshi Bar .
Wakati huo huo Meya Kumbilamoto alisema Halmashauri ya Jiji imepokea shilingi Bilioni 6 kwa ajili ya miradi ya Maendeleo wilaya ya Ilala ikiwemo sekta ya Elimu .
Alitumia nafasi hiyo kupongeza Shirika la Sauti ya JAMII Kipunguni kwa kuwaunganisha Vijana pamoja katika shughuli za ushonaji ,Kilimo Cha Mbogamboga ,ujasiriamali na usaidizi wa kisheria kupinga Ukatili wa kijinsia na kiwanda cha Mkaa.
Aliwataka Vijana wa wilaya ya Ilala wasijiunge katika makundi hatarishi ya Panya road badala yake amewataka wajiunge katika vikundi vya Maendeleo ambayo vina faida kwa Jamii’.
Mwisho