Home LOCAL KAJENJELE YAZINDUA GARI ZA USAFI ZA KISASA ILALA

KAJENJELE YAZINDUA GARI ZA USAFI ZA KISASA ILALA

Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam Amos Makala akizindua gari za kisasa za Usafi Halmashauri ya Jiji Dar Es salaam Leo Septemba 24 Jumamosi ya Mwezi wa usafi magari hayo ya Kampuni ya Kajenjele wengine Viongozi wa Mkoa na Wilaya ya Ilala (Picha na Heri Shaaban )

Mkuu wa Mkoa wa Dar Es salaam Amos Makala ,na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Arc,Ng’wilabuzu Ludigija (katikati) na Diwani wa Kata ya Kivukoni wa kwanza Kushoto Sharik Choughule wakiwa katika Kampeni endelevu ya pendezesha Dar es Salaam Wilayani Ilala Leo Septemba 24/2022 Viwanja vya Mnazi Mmoja (PICHA NA HERI SHAABAN))

Na: Heri Shaaban (Ilala)

Kampuni ya Usafi ya Wilayaji Ilala Dar es Salaam Kajenjele imezindua magari ya kisasa ya usafi kwa ajili ya kusafisha na kuipendezesha Dar es Salaam iwe ya kisasa .

Akizungumza wakati wa kuzindua gari za taka Mkurugenzi wa Kajenjele ,Methew Andrew, alisema juhudi za kampuni yake Kajenjele katika uzinduzi wa gari hizo kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano ,Samia Suruhu Hassan, Dar es Salaam iwe Jiji la Utalii barani Afrika kwani ni sehemu ya kitovu cha Biashara na sekta ya uchumi .

“Katika kuunga mkono juhudi za Serikali na kuipendezesha Dar Salaam magari tuliozindua yana uwezo wa kubeba Tani 26 za takataka kwa sasa barani Afrika tumeshika nafasi ya kwanza kwa usafi mikakati yetu Dar es asalaam kushika nafasi ya kwanza kwa usafi uwezo wanao tutashirikiana na Serikali pamoja na Halmashauri ya Jiji katika kuipendezesha Dar Salaam” alisema Kajenjele.

Alisema gari hizo za taka taka zitawekwa sehemu maalum ambayo Wananchi wanazalisha takataka kazi yake kubwa kukusanya takataka .

Alisema kampeni ya Kajenjele imewekeza Dar Salaam na Morogoro kwa ajili ya Shughuli za usafi kuisaidia Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Watanzania kila sekta imetoa ajira kwa vijana na Wanawake Ili waweze kukuza uchumi na kuingizia kipato cha kusomesha watoto wao

Mikakati ya Kampuni ya Kajenjele wamejipanga Ilala iwe safi Kila mmoja awe BALOZI wa Mwezake katika sekta ya usafi na Mazingira .

Amepongeza Serikali ,Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam,Ofisi ya Mkuu wa Wilaya na Mkuu wa Mkoa kwa kumpa ushirikiano katika utekelezaji wa Majukumu yake kazi .

Mwisho.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here