Mkurugenzi wa Jiji hilo la Dar es Salaam AMANI MAFURU akizungumza alipokuwa akifungua rasmi kikao cha Idara ya Elimu sekondari cha Utekelezaji wa mwongozo wa viongozi na mikakati ya uimarishaji ufundishaji na ujifunzaji kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji AMANI MAFURU akiongea na Walimu Wakuu wa Shule za Sekondari Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam katika Kikao Cha Idara ya Elimu Sekondari Cha Utekelezaji wa mwongozo wa uteuzi wa viongozi na mikakati ya uimarishaji na ufundishaji na ujifunzaji ngazi ya Elimu Msingi na Sekondari Wilayani Ilala Leo Septemba 01/2022 (Picha na Heri Shaaban)
Walimu Wakuu wa Shule za Sekondari Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam wakiwa katika Kikao Cha Idara ya Elimu Sekondari Cha Utekelezaji wa mwongozo wa uteuzi wa viongozi na mikakati ya uimarishaji na ufundishaji na ujifunzaji ngazi ya Elimu Msingi na Sekondari Wilayani Ilala Leo Septemba 01/2022 (Picha na Heri Shaaban )
Na: Heri Shaaban (Ilala)
HALMASHAURI ya Jiji la Dar es Salaam yawapatia mafunzo walimu wake wa idara Elimu Sekondari wa shule za Serikali na za binafsi .
Akifungua kikao cha Idara ya Elimu sekondari cha Utekelezaji wa mwongozo wa viongozi na mikakati ya uimarishaji ufundishaji na ujifunzaji ngazi ya elimu msingi na sekondari kaimu Mkurugenzi wa Jiji hilo la Dar es Salaam AMANI MAFURU, amewataka Walimu kuakikisha wanafunzi wanafaulu kwa kila Somo lao Darasani Ili kuongeza taaluma bora Wilayani Ilala.
“Naomba Walimu wakuu maafisa elimu kata kushirikiana na Walimu na Wazazi katika taaluma shuleni kuakikisha kila Mwalimu wa Somo Mwanafunzi wake anapata alama za juu ili Wilaya yetu iweze kufanya vizuri lazima tuanze na mikakati ya kushirikiana katika sekta ya Elimu “ alisema MAFURU.
Kaimu Mkurugenzi MAFURU alisema walimu ni viongozi Bora wa kesho kazi yao wanayofanya Serikali inatambua pia miongoni mwao kuna Wakurugenzi hivyo wafanye kazi kwa weledi bila kuvunjika moyo.
Alipongeza Idara Elimu sekondari kwa kuandaa mwongozo wa elimu kwa ajili ya shule za sekondari binafsi na za Serikali .
Amewataka Wakuu wa Shule kufanya vikao kila wakati na Wakuu wa bodi ya shule pamoja na kuwashirikisha MAAFISA elimu kata kujua changamoto zao Ili Serikali iweze kuzipatia ufumbuzi wake
Kwa upande wake Afisa Elimu Sekondari Mwalimu Mussa Ally, alisema dhumuni la kikao kuweka mikakati ya mpango ya utekelezaji idara ya Elimu Sekondari kwa Shule binafsi na za Serikali kwa ajili ya kupanga mikakati katika sekta elimu Idara ya Elimu Sekondari .
Mwalimu Mussa alisema katika sekta ya Elimu kitaaluma Halmashauri ya Jiji inajivunia kitaaluma mafanikio makubwa katika taaluma pamoja na Michezo kila mwaka inafanya vizuri .
Alisema kwa Sasa Halmashauri ya Jiji ina shule za Sekondari 114 za Serikali 63 binafsi Shule 50.
Mwalimu Mussa amewataka walimu wakuu kufanya kazi kwa kushirikiana pamoja Ili malengo sekta ya Elimu Sekondari yafikie malengo yake ikiwemo kuongeza ufaulu Kwa Shule zake.
Mwalimu Mkuu wa Tambaza Sekondari Hussein Zuberi amewataka wakuu wa Shule kusimamia sekta ya Elimu Idara ya Elimu Sekondari kwa Shule za serikali na binafsi kwa pamoja wanavyopanga mikakati ya ufaulu .
Mwisho.