Home Uncategorized WAKAZI WA NYAMALIMBE, LWAMGASA WALIA NA LATRA ZUIO LA MAGARI MADOGO...

WAKAZI WA NYAMALIMBE, LWAMGASA WALIA NA LATRA ZUIO LA MAGARI MADOGO MAARUFU MICHOMOKO.

Wananchi wa kijiji cha Lwamgasa wilayani Geita wakisubilia usafiri katika kitu o cha Lwamgasa.

Jackline Joseph akizungumza na wandishi wa habari katika kijiji cha Lwamgasa

Kaimu afisa mfawidhi wa Mamlaka ya udhibiti usafirishaji ardhini (LATRA) Mkoa wa Geita Maria CHACHA.

Na: Costantine James, Geita.

Wakazi wa Kijiji cha Lwamgas na Nyamalimbe wilayani Geita Mkoani Geita wameiomba serikali kuingilia kati  changamoto ya ukosefu wa usafiri  katika maeneo yao hali inayowalazimu kutumia usafiri wa Pikipiki maarufu kama bodaboda hali inayopelekea kuhatalisha maisha yao.

Wamebainisha hayo leo mkoani Geita wakati wakizungumza na waandishi wa habari katika maeneo yao wamesema, changamoto ya ukosefu wa usafiri katika maeneo hayo, imekuja baada ya serikali kupitia Mamlaka ya udhibiti usafiri ardhini (LATRA) kuzuia magari madogo aina ya mchomoko kusafirisha abilia katika maeneo yao.

Magari hayo yalikuwa yakifanya safari kutoka Katoro  nyamalime,Katoro Lwamgasa, katoro Nyakabale na Katoro Nyarugusu yamezuiliwa kutoka na kutokuwa na leseni ya usafirishaji abilia kutoka kituo kimoja kwenda kingine katika maeneo hayo.

Wananchi hao wamesema zuio hilo limewaathili pakubwa kutokana na kukosa usafiri hivyo kushindwa kufanya shughuli zao mbalimbali za uzalishaji kwani magari makubwa yenye leseni za kufanya usafirishaji hayakidhi mahitaji yao.

“Kwa kweli kutokana na changamoto ya kuzuiliwa kwa magari imetuathili sisi wafanyabiashara wadogo ambao tulikuwa tukisafirisha mizigo yetu kutoka katoro na kuleta Lwamgasa sasa magari yamekosekana na jinsi ya kubebe kwenye pikipiki inakuwa ni changamoto sana tunaomba magari yaruhusiwe ilikusudi shughuli za kila siku ziweze kuendelea” alisema Jackline Joseph mkazi wa Lwamgasa.

Kwa upande wake Kaimu afisa Mfawidhi wa Mamlaka ya udhibiti usafirishaji ardhini (LATRA) Mkoa wa Geita  Maria  P. Chacha amesema wao hawajawazuia magari  hayo kufanya kazi zao kwa mjibu wa Leseni zao.

Maria amesema leseni za madereva hao zinawataka kukodiwa kutoka kituo kimoja kwenda kingine na sio kusafirisha abiria kutoka ruti moja kwenda nyingine kwani kufanya hivyo ni kosa kisheria na wanakiuka mashariti ya leseni zao.

Amewataka kufata sheria na taratibu kwa mjibu wa leseni zao ili kuondokana na changamoto hiyo wanayoipata kwani kila kitu kinaongozwa na kanuni na sheria hivyo wafanye kazi kama leseni zao zinavyo wataka kinyume na hapo ni uvunjifu wa sheria.

“Maeneo yanayolalamikiwa ni katoro Lwamgasa, katoro  Nyamalimbe, katoro Nyakabale na Katoro Nyarugusu hayo maeneo yote tumeyapitia nakuona hayo malalamiko yao kimsingi sisi hatujawazuia kufanya kazi zao tumewaambia wafate sheria, kanuni na taratibu kutokana na leseni zao leseni zao haziwataki wao wafanye kama wanavyofanya saivi wanafanya kazi za ruti ambapo wanaingilia usafiri wa hizi haice na Costa kwenye maeneo yale wenyewe wanatakiwa wakodiwe katika maeneo wanayoyafanya kazi” alisema Maria  P. Chacha  Kaimu afisa Mfawidhi wa LATRA Mkoa wa Geita .

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here