Home LOCAL TATIZO LA ELIMU TASNIA YA HABARI KUMALIZWA

TATIZO LA ELIMU TASNIA YA HABARI KUMALIZWA

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), amesema suala la elimu katika tasnia ya habari, linatafutiwa mwarobaini.

Amesema, wanapendekeza waandishi waliopo kwenye tasnia ya habari ambao hawajafikisha vigezo, wasiondolewe na badala yake wapate mafunzo wakiwa kazini, huku wanaoingia lazima wakidhi vigezo vya elimu iliyoweka.

Balile ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na mtangazaji Abdallah Kurwa katika Kipindi cha Kumepambazuka kinachorushwa na Radio One tarehe 10 Agosti 2022.

Tungependa waandishi waliopo kazini wasiondolewe bali wapate mafunzo wakiwa kazini, lakini wale wapya wanaotaka kuingia katika tasnia ya habari, lazima wakizi vigezo vya kuwa na elimu walau Diploma,” amesema Balile, Mwenyekiti wa TEF.

Amesema, sio kila anayeweza kusoma na kuandika anaweza kuwa, na kwamba uandishi ni taaluma iliyo na misingi yake.

Kuna kipaji na taaluma, ukiwa na kipaje basi lazima upate misingi ya taaluma hapo unakuwa mwandishi mzuri, kila taaluma ina misingi yake,” amesema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here