Home LOCAL ‘MLETE MZUNGU’ NI KAULI ZA MASHABIKI WA SIMBA SC KWA KUIPIGA KAGERA...

‘MLETE MZUNGU’ NI KAULI ZA MASHABIKI WA SIMBA SC KWA KUIPIGA KAGERA 2 -0

Klabu ya Wekundu wa SIMBA SC leo wameendeleza vichapo kwa kuitandika timu ya kagera Sugar mabao 2-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania bara uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Mshambuliaji Mosses Phiri ndie alikuwa wa kwanza kuipatia Simba bao la kuongoza katika dakika ya 42 ya mchezo huo alipomalizia mpira wa adhabu uliogonga besera na kururudi uwanjani mpira uliopigwa na kiungo machachari Clautus Chama.

Dejan Georgijevic aliamsha shangwe za mashabiki wa Simba baada ya kuipatia timu yake bado la pili na la ushindi katika dakika ya 81 lililoipa ushindi Simba wa jumla ya mabao 2 – 0 katika mchezo huo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here