Home LOCAL JUMUIYA YA WAZAZI WILAYA YA ILALA YAELEZA FAIDA ZA SENSA

JUMUIYA YA WAZAZI WILAYA YA ILALA YAELEZA FAIDA ZA SENSA

Meya wa Halmadhauri ya Jiji la Dar es Salaam Omary Kumbilamoto akizungumza katika Kongamano la Sensa ya watu na Makazi lililoandaliwa na Taasisi ya Fahari Tuamke Maendeleo Leo Agosti 20/22 Chanika Mtaa wa YONGWE (Kushoto)Mwenyekiti wa CCM Chanika William Mwila (Picha na Heri Shaaban)

Mkurugenzi wa Fahari Tuamke Maendeleo Neema Mchau akizungumza katika Kongamano la Sensa lililoandaliwa na Taasisi yake ya Fahari (Picha na Heri Shaaban)

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM kata ya Chanika William Abas Mwila akisalimiana na Meya wa Halmashauri ya Jiji Omary Kumbilamoto katika kongamano la Sensa kutoa elimu kwa Wananchi wa Mtaa wa YONGWE Kata ya Chanika kongamano hilo limeandaliwa na Fahari Tuamke Maendeleo Leo 20/08/2022 (PICHA NA HERI SHAABAN)

Afisa Mtendaji wa Chanika Charles Kimario akitoa Elimu ya Sensa ya Watu na Makazi kwa niaba ya Mratibu wa Sensa Wilaya ya Ilala Mtaa wa YONGWE Chanika katika Kongamano la Sensa lililoandaliwa na Fahari Tuamke Maendeleo (katikati)Mwenyekiti wa CCM Chanika William Abas Mwila na Meya wa Halmashauri ya Jiji Omary Kumbilamoto (PICHA NA HERI SHAABAN)

Wanafunzi wa Fahari Day Care Center wakiwa na Mabango ya kuhamasisha Sensa katika Kongamano la Sensa lililoandaliwa na Fahari Tuamke Maendeleo Leo Agosti 20/2022 Viwanja vya YONGWE Chanika (PICHA NA HERI SHAABAN)

Na Heri Shaaban (Ilala)

Kamati ya Utekelezaji Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Ilala yaeleza faida za SENSA ya Watu na Makazi kwa Wananchi wake.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Ilala Mohamed Msophe alisema Sensa ya Watu na Makazi ina FAIDA nyingi katika nchi yetu ikiwemo Maendeleo ya Taifa.

“Tamko letu Kamati ya Utekelezaji Jumuiya ya Wazazi kwa Watanzania tushiriki kuhesabiwa siku ya Agosti 23 2022 mwaka huu Ili Serikali iweze kupanga malengo yake na kujua idadi ya Watanzania kwa ujumla ni lazima tuhesabiwe” alisema Msophe .

Msophe aliwataka viongozi wa Jumuiya chama na Jumuiya kuanzia ngazi ya matawi na Kata kutoa elimu kwa Wananchi kwa ajili ya siku Maalum ya Agosti 23 kila mtu atoe ushirikiano kwa makarani wa sensa watakaopita nyumbani kwako siku ya kuamkia Agosti 23/2022 Ili muweze kuhesabiwa.

Msophe alisema Ili Serikali iweze kupanga malengo yake ya kipindi cha miaka mitano lazima kwanza iweze kujua Idadi ya Watanzania kwa ujumla ndio iweze kupanga bajeti mbalimbali ikiwemo za Huduma za Jamii ikiwemo sekta ya Afya ,sekta ya Elimu miundombinu .

Aidha alisema Sensa ya watu na Makazi itasaidia serikali kujuwa jinsi gani ya kuhudumia wananchi wake kutokana na idadi yao

Pia Mwenyekiti Msophe ameshauri wananchi kutokuwaficha hata watoto ambao ni walemavu ili serikali kupata idadi yao ili kujipanga jinsi ya kuwasaidia, pia sensa itasaidia serikali kusogesa mipango mbalimbali kwenye maeneo mbalimbali kama kusogeza huduma za wananchi karibu kutokana na idadi ya watu watakaopatikana katika sensa ya 2022.

Mwisho.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here