TANGA.
Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), inaendesha mafunzo ya siku tano Jijini Tanga, kwa Maafisa Biashara kuhusu Sheria ya Leseni za Biashara.
Maafisa hao wanaopatiwa mafunzo ni kutoka mikoa ya Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara.
Mkurugenzi wa Leseni wa BRELA Bw. Andrew Mkapa, akiwakaribisha katika mafunzo hayo amesema lengo kuu ni kuwajengea uwezo na uelewa juu ya utekelezaji wa Sheria ya Leseni za Biashara ambayo wakiielewa vizuri itawasaidia katika utekelezaji wa majukumu yao, ikiwa ni pamoja na kutoa usaidizi kwa wadau wanaohitaji leseni za biashara katika maeneo yao.
Mafunzo haya yaliyoanza tarehe 15 Agosti, 2022 yatahitimishwa tarehe 19 Agosti,2022