Home BUSINESS ATAKAYEHUJUMU JUHUDI ZA SERIKALI MBOLEA ZA RUZUKU KUCHUKULIWA HATUA

ATAKAYEHUJUMU JUHUDI ZA SERIKALI MBOLEA ZA RUZUKU KUCHUKULIWA HATUA

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Dkt. Stephan Ngailo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano wa mamlaka hiyo Temeke Jijini Dar es Salaam leo tarehe 20 Agosti, 2022.
DAR ES SALAAM.

Atakayebainika kuhujumu juhudi za serikali ya Awamu ya Sita ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kutoa ruzuku ya mbolea ili kuwapunguzia wakulima mzigo wa bei kubwa ya mbolea atachukuliwa hatua kali.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Dkt. Stephan Ngailo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano wa mamlaka hiyo Temeke Jijini Dar es Salaam leo tarehe 20 Agosti, 2022.

Wito huo umekuja siku chache baada ya taarifa za viongozi na watumishi wanaosajili wakulima Wilaya ya Wanging’ombe Mkoani Njombe kuwasajili wakulima kwa kuwatoza kiasi cha fedha jambo ambalo ni kinyume cha taratibu za usajili wa wakulima unaoendelea nchi nzima.

“Hakuna mkulima yeyote anayetakiwa kutoa kiasi chochote cha fefha kwa ajili ya kujisajili ili kunufaika na mbolea za ruzuku ni bure, na usajili huu ni endelevu” anasisitiza Dkt. Ngailo.

Dkt. Ngailo amemshukuru Mkuu wa Wilaya ya Wanging’ombe kwa kukemea jambo hilo kwa nguvu zake zote mara tu alipopata taarifa hizo.

Aidha, Dkt. Ngailo amewatoa hofu wakulima ya kutokupata mbolea na kubainisha kila mkulima atakayesajiliwa atapata mbolea za ruzuku bila shida yeyote.

Amesema kwa sasa upatikanaji wa mbolea ni mzuri na kuwa kwa mwezi Julai jumla ya tani laki moja na ishirini na sita elfu za mbolea zilikuwepo kwenye maghala mbalimbali ya mbolea nchini.

Ameongeza kuwa mwezi huu wa nane meli nyingi zimeingia na shehena za mbolea meli itakayoingia leo ina zaidi ya tani elf 23 za mbolea mbalimbali za NPK tarehe 25 Agosti meli nyingine itaingia ikiwa na tani elf 30 za mbolea ya DAP na NPKz na meli nyingine yenye tani 17 itaingia tarehe 2Septemba, 2022 huku meli nyingine zitaingia mwezi septemba zikiwa na shehena za kutosha za mbolea.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here