TEF imemkumbusha Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye kuongeza kasi ya mchakato huo kama alivyoahidi.
Deodatus Balile, Mwenyekiti wa TEF, akizungumza leo jijini Dar es Salaam amesema, kasi ya mchakato wa mabadiliko ya sheria hizo, kwa sasa umepoa hivyo kutia shaka mafanikio ya tamati ya mchakato huo ndani ya mwaka huu.
“Rais amekuwa akitoa msukumo mkubwa sana ili kuhakikisha wanashirikisha wadau wa habari na serikali kuhakikisha sheria zinarekebishwa. Tulikwenda vizuri hapo mwanzo, lakini tangu baada ya Mei 3 mwaka huu (Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani), tunaona kama kasi imepungua kidogo.
“Tungependa kujua. Wizara ilikuwa imepanga kufanya mikutano kadhaa na kujadiliana na wataalamu wa tasnia hii, lakini sasa tunaona kama kila kitu kimesimama na tunapoendelea kuuliza, tunaambiwa bado mikutano ipo,” amesema Balile.
Mwenyekiti huyo wa TEF amesema, mabadiliko ya sheria hizo bado ni muhimu kwa mazingira yua sasa huku akipendekeza kasi ya mabadiliko hayo ili kuwa Bunge la Novemba kwa kuwa ndio bunge la miswada.
“Bado tunazihitaji sheria, bado tunahitaji hayo mabadiliko haraka kadri inavyowezekana kuliko wakati wowote ule kwa sababu, tukipitwa na lile bunge la mwezi wa tisa, ina maana tutasubiri mwaka mmoja baadaye. Bunge la mwezi wa tisa ndio la miswada,” amesema.
Pamoja na kuchelewa huko, Balile amasema iwapo wizara uenye dhamana ikiamua sasa kuongeza kasi katika mchakato huo, upo uwezekano mkubwa wa kufikia malengo ndani ya muda muafaka.
“Tunachotafuta zaidi ni haki ya kupata habari na uhuru wa vyombo vya Habari. Huu uhuru unawezesha haki nyingine kupatikana. Mfano demokrasia na vingine vyote vinavyozungumzwa, vinatokana na uhuru wa watu kutoa mawazo yao.
“Inapokuwa uhuru haujalindwa kisheria, basi unachelewesha hivi vingine kupatikana katika jamii. Huu ni mjadala na mchakato tunaopaswa kushirikishana tulio wengi kwa Pamoja,” amesema.
Hata hivyo, Nape akizungumza katika Mkutano wa Wadau wa Maendeleo kusaidia ukuaji wa habaro tarehe 13 Julai 2022 alisema, serikali imetoa nafasi kwa wanahabari kuwasilisha mbadala wa maoni yao na kwamba, na ina malengo ya kuukamilisha mchakato huo kwa muda mfupi.
“Serikali imetoa nafasi kwa wanahabari kuleta mbadala wa yale yanayolalamikiwa, tukae mezani tuzungumze na huo mchakato haiwezi kuwa mfupi, ni chakato wa mazungumzo, mie nimeukuta na tuaendelea nao. Tuna malengo ya kuukamilisha mapema kadri inavyowezekana,” alisema Nape na kuongeza;
“Sheri ya habari ilipotungwa, ililenga kutatua matatizo ya habari ikiwemo ajira zao, maslahi yao, mazingira yao ya kazi, haki zao na wajibu wao. Sasa inawezekana masuluhisho yaliyopo kwenye sheria, ndio yanayogombaniwa kwamba ni sahihi ama si sahihi.”
Alsiema, lengo la mchakati wa sasa ni kutengeneza sheria zitakazodumu kwa muda mrefu na ambazo zitakubalika katika pande zote mbili (serikali na wadau) pia zitakazotengeneza mazingira kuwa bora zaidi kuliko ya sasa.
Gerson Msigwa, Msemaji Mkuu wa Serikali alisema,
Suala la Bodi ya Ithiibati, hayo ni miongoni mwa mambo yanayokwenda kujadiliwa kwenye mchakato mzima wa kupitia upya sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari namba 12 ya mwaka 2016 ambayo ndio imeunda hiyo Bodi ya ithibati
Ninachotaka kusema ni kwamba, serikali imeonesha dhamira sasa kwamba tunataka kwenda kupitia upya sheria na taratibu zote zilizowekwa kwa mujibu wa Sheria ya Huduma za Habari.
Wadau wameonesha nia ya kushirikiana na serikali, wadau na waandishi wa habari katika kuhakikisha tunaweka vizuri mazingira ya waandishi wa habari na vyombo vya habari.