Home LOCAL SERIKALI YATOA BILIONI 1 KUMALIZA KERO YA MAJI KATA YA NKOME NA...

SERIKALI YATOA BILIONI 1 KUMALIZA KERO YA MAJI KATA YA NKOME NA KATOMA GEITA.



Na.Costantine James, Geita.

Wananchi wa kijiji cha Nkome Kata ya Nkome wilayani Geita mkoani Geita wameishukuru Serikali kupitia kwa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Wilaya ya Geita kwa kuwapelekea Mradi wa Maji katika Kata ya Nkome Utakao wawezesha kupata Maji safi na Salama hali itakayosaidia Kuachana na Matumizi ya Maji ya ziwani.

Wananchi hao wamesema Wanashukuru kwa mradi wa Maji  katika eneo lao kutokana na kasi ya ujenzi Unavyoendelea katika mradi huo unaosimamiwa na Wakala wa maji safi na usafi wa mazingira vijijini (RUWASA) wilaya ya Geita kwani utawawezesha kupata maji safi na salama kwa urahisi zaidi.

Wamesema matumizi ya Maji kutoka ziwa Victoria yamekuwa na Madhara makubwa ya kiafya kwa wakazi  hao kutokana na kusababisha Magonjwa mbalimbali ikiwemo  Kutapika damu, kichocho, Kuhara, Magonja ya tumbo yanayosababishwa na matumizi ya maji ya ziwani Ambayo sio safi na salama hivyo mradi huo ni mkombozi kwa wakazi wa Kata ya Nkome na Katoma.

Diwani wa Kata ya Nkome Masumbuko Mulebesi amesema Mradi huo Pindi utakapokamilika utakwenda kutatua kero ya upatikanaji wa maji safi na salama katika Kata ya Nkome na Vitongoji vyake.

Mhe, Masumbuko amesema kutokana na wakazi wa Nkome kutumia Maji ya Ziwa Victoria kumekuwa na changamoto Mbalimbali zinazojitokeza ikiwemo watoto kuliwa na Mamba, Kutapika damu, pamoja na wakazi kuzama ziwani wakiwa wanaoga.

Amesema Mradi huo utakapo Kamilika utapunguza Changamoto ya Upatikanaji wa Maji safi na Salama pamoja na Kupunguza Gharama Kutokana na Wakazi hao Kununu Maji ya kisima kwa Gharama kubwa kwani ndoo Moja ya maji lita 20 Wananunua kwa 1000 hivyo Mradi huo Utasaidia kuwatua Wakina mama ndoo Kichwani.

Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira vijijini (RUWASA) Wilaya ya Geita Mhandisi Sande Batakanwa amesema Mradi huo Unahusisha Kata tano ambazo ni Nkome, Katoma, Nyamboge, Nzera, na Lwezera zilizopo ndani ya Wilaya ya Geita.

Mradi huo unaghalimu kiasi cha bilioni 1 mpaka kukamilika kwake na pindi utakapo kamilika utamaliza kero ya ukosefu wa maji safi na salama kwa wakazi wa Geita vijijini na kutimiza adhima ya serikali ya kumtua ndoo mama kichwani pamoja na kupunguza mda wa kufata maji.

Amesema kutokana na bajeti iliyopo kwa sasa wameamua kuanza kutekeleza mradi huo katika kata Mbili Kata ya Nkome na Katoma huku kipaumbele kikubwa ikiwa ni Kata ya Nkome kutokana na kuwa na wakazi wengi wenye uhitaji wa maji safi na salama kwa haraka Zaidi.

Mhandisi Sande amesema wameamua kuanza na Kata ya Nkome kutokana na wananchi wa kata hiyo kutumia maji ya ziwa ambayo yanahatalisha afya zao kwani maji hayo yamekuwa chanzo cha magojwa  mbalimbali ikiwemo Magojwa ya tumbo, kuhara pamoja na kushambuliwa na mamba pindi wanapoenda kuchota maji ziwani.

Mradi huo umefikia asilimia 60% ya utekelezwaji wake katika kata ya Nkome na Katoma na pindi utakapokamilika utahudumia wananchi zaidi ya 46,415 kutoka katika kata tano zilizopo jimbo la Geita vijijni ndani ya wilaya ya Geita.

Mhandisi Sande amesema mradi huo unahusisha ujenzi wa chanzo cha maji, sehemu ya kutibu maji, ufungaji wa pampu 4, ujenzi wa matanki 4 ambapo mawili kila kata  Nkome na Katoma yenye ujazo wa lita 225,000, ujenzi wa vituo vya kuchotea maji 30 vya umma pamoja na kutandaza mabomba eneo la kilomita 64km.

Sande amemushukuru mbunge wa jimbo la Geita vijijini DK. Joseph Kasheku Msukuma kutokana na ushirikiano wake katika utekelezaji wa mradi  huo Pamoja na serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kupitia wizara ya maji kwa kuwezesha kupatikana kwa fedha ambazo zinatekeleza mradi huo kwa lengo la kuondoa kero ya  ukosefu wa maji safi na salama kwa wananchi.

“Nimshukuru mhe, waziri wetu anafanya kazi kubwa viongozi wetu wote wa pale wizarani wamesaidia sana mpaka kupata hizi fedha na kuweza kutekeleza mradi mkubwa kama huu ni kweli fedha hizi zinzhitajika maeneo mengi tu hawajapata huduma lakini mpaka sisi tunatengewa bilioni moja ni jambo kubwa sana.

“kwa kipekee nipende kumshukuru Mhe, Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mama yetu Samia Suluhu Hassani anafanya kazi kubwa pamoja na mradi huu tunaoujenga lakini bado kuna mradi ambao unajegwa unaotoka huku kwenye jimbo la mhe, Msukuma kutoka Senga mchangani unapeleka maji Geita mjini mradi ule tuliemda kuhudhulia pale ikulu wamesainishwa  mkandarasi ameshakuja saiti na kazi ianendelea.

“kwahiyo mimi niseme ukweli kwa upande wa Mhe, Rais amekuja kutatua kero ya maji katika nchi hii miradi mingi sana inafanyika mimi kwangu tu nina miradi kalibia 9 inaendelea na ujenzi” Amesema Mhandisi Sande Batakanwa Meneja Ruwasa Wilaya ya Geita.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here