Home BUSINESS RAIS DKT. MWINYI ATEMBELEA MAONESHO YA 46 YA BIASHARA YA SABASABA JJINI...

RAIS DKT. MWINYI ATEMBELEA MAONESHO YA 46 YA BIASHARA YA SABASABA JJINI DAR


DAR ES SALAAM.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt Hussein Ali Mwinyi ameipongea  Wizara ya Uwekezaji na Biashara kwa kuanzisha  Mfumo wa kielektroniki wa huduma za pamoja kwa wawekezaji  na programu ya  utengenezaji wa mashine mbalimbali  zinazowezesha uanzishaji wa viwanda .

Rais Mwinyi ameyasema hayo Julai 04 2022 alipotembelea Banda la Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara  nakujionea  Mfumo wa kielektroniki wa huduma za pamoja kwa wawekezaji  na mashine mbalimbali zinazoweza  kutumika kuanzisha kiwanda kuanzia milioni sita  hadi  milioni 600. 

Rais Mwinyi amesema hii ni hatua nzuri kwani hata nchi zilizoendelea zilianza kutengeneza mashine kama hizi  na sasa zinatengeneza mashine na mitambo mikubwa. Natumaini mwakani mtakuwa na maendeleo makubwa ya mashine hizo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here