Home LOCAL MUHAS YADAHILI WANAFUNZI ZAIDI YA ELFU 9 TANGU KUFUNGULIWA KWA DIRISHA HILO

MUHAS YADAHILI WANAFUNZI ZAIDI YA ELFU 9 TANGU KUFUNGULIWA KWA DIRISHA HILO

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Dk. Francis Michael akimsikiliza Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili  (MUHAS) Profesa Andrea Pembe wakati akitoa maelezo katika Banda Hilo kulia ni Afisa Habari na Mawasiliano (MUHAS) wakati kiongozi huyo ametembelea katika Banda la Chuo hicho kwenye maonesho ya 17  ya Vyuo Vikuu yaliyoandaliwa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania TCU na kufanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam,   Maonesho hayo yamefungwa rasmi leo.

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Dk. Francis Michael na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili  (MUHAS) Profesa Andrea Pembe wakimsikiliza Afisa Habari na Mawasiliano (MUHAS) wakati waliotembelea katika Banda la Chuo hicho kwenye maonesho ya 17  ya Vyuo Vikuu yaliyoandaliwa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania TCU na kufanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam,   Maonesho hayo yamefungwa rasmi leo.

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Dk. Francis Michael akisaini kitabu wakati alipotembelea Banda la Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili  (MUHAS)katika maonesho ya 17  ya Vyuo Vikuu yaliyoandaliwa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania TCU na kufanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam,   Maonesho hayo yamefungwa rasmi leo.

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Dk. Francis Michael akipokea zawadi kutoka Kwa John Helman Mfamasia Msaidizi katika taasisi ya Dawa ya Asili Muhimbili (MUHAS) wakati waliotembelea katika Banda la Chuo hicho kwenye maonesho ya 17  ya Vyuo Vikuu yaliyoandaliwa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania TCU na kufanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam,   Maonesho hayo yamefungwa rasmi leo.

Na: Hughes Dugilo, DAR.

Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kimesema kuwa tangu kufunguliwa kwa Dirisha la Udahili wa wanafunzi wa Elimu ya Juu Chuo hicho kimefanikiwa kudahili wanafunzi zaidi ya elfu tisa.

hayo yamebainishwa na Afisa Uhusiano wa Chuo hicho Neema Edwin katika mahojiano maalum na waandishi wa habari wakati wa kufunga rasmi Maonesho ya 17 ya Elimu ya Juu sayansi na Teknolojia yalimalizika leo Julai 23,2022 katika viwanja vya mnazi mmoja Jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa Chuo hicho kimeshiriki kwa mafaniko makubwa maonesho hayo ambapo pamoja na mambo mengine kimepata fursa ya kutembelewa na watu wengi hususani wanafunzi wanaotaka kujiunga na Chuo hicho ambapo pamoja na mambo mengine walifanya udahili wa papo wa hapo katika maonesho hayo.

Adha  idadi hiyo ya wanafunzi zaidi ya elfu tisa imejumuisha na wale waliodahiliwa katika maonesho hayo na kwamba wanafunzi wanaoomba kujiunga na Chuo hicho wanaendelea kufanya maombi ya moja kwa moja kupitia mtandao wa Chuo hicho wa www.oac.muhas.ac.tz ambapo kwa kupitia tovuti hiyo mwanafunzi anaweza kujisajili mwenye akiwa mahali popote.

“Katika maonesho haya tumetembelewa na watu zaidi ya 500 ambao wamefika hapa kupata maelezo mbalimbali juu ya chuo chetu na wengi wao wamefanya udahili wa moja kwa moja  hapa”  Amesema Neema.

Maonesho ya 17 ya Elimu ya Juu Sayansi na Teknolojia yaliyoandaliwa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) yalifunguliwa rasmi na Waziri Mkuu Kassim majaliwa Majaliwa  Julai 18 ambapo leo Julai 23,2022 yamefungwa rasmi na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Dkt. Francis Maiko.
Previous articleWASHIRIKI WA MKUTANO WA WIPO USWISI WATEMBELEA UBALOZI
Next articleCHUO KIKUU CHA MBEYA CHA SAYANSI NA TEKNOLOJIA (MUST) CHAPONGEZWA KWA UBUNIFU
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here