Home LOCAL MRADI WA BARABARA MUSOMA WAKATALIWA KUZINDULIWA

MRADI WA BARABARA MUSOMA WAKATALIWA KUZINDULIWA

Makabidhiano ya Mwenge kati ya Wilaya ya Musoma na Mqnispaa ya Musoma.

JIWE lililoandaliwa kwa uzinduzi wa Barabara ya Mkirira – Kwangwa, Mkirira – Zahanati (Km. 6.3), Musoma (DC), Mkoa wa Mara liking’olewa.

 Zahanati ya Mkirira ambayo iliwekewa Jiwe na Msingi na Kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa Mwaka huu,  Sahili Nyanzabara Geraruma, wilayani Musoma.

Na: Editha Majura: MUSOMA.

BARABARA ya Mkirira – Kwangwa na Mkirira Zahanati yenye Km 6.3 katika Halmashauri ya Wilaya ya Musoma, mkoani Mara imeshindikana kuzinduliwa kutokana na Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini – Tanzania (TARURA), kutotekeleza maagizo ya Mwenge wa Uhuru.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2022, Sahili Nyanzabara Geraruma katika kila halmashauri mazungumzo yake ya awali yamekuwa yakielekeza nyaraka zote, vifaa vya kupimia na wataalamu wote wa miradi  iliyoandaliwa kukaguliwa, wakutwe eneo la mradi lakini TARURA hawakuwewa na vifaa vya kukagulia barabara hiyo na hivyo Jiwe la Msingi lililotakiwa kuzindulia mradi huo uliyojengwa kwa Sh Milioni 312.65 za maendeleo ya Mfuko wa Barabara (Road Fund), liling’olewa, likachukuliwa na Mwenge.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here