Home BUSINESS BRELA YAIBUKA MSHINDI WA PILI MAONESHO YA SABASABA

BRELA YAIBUKA MSHINDI WA PILI MAONESHO YA SABASABA

Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), imeibuka mshindi wa pili katika kipengele cha  Uhamasishaji, Uwezeshaji  Biashara na Uwekezaji huku Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ikishika nafasi ya kwanza na  Chama  cha Wafanyabiashara wenye Viwanda na Wakulima Tanzania (TCCIA) ikichukua nafasi ya tatu,  katika  Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa yaliyofanyika katika viwanja vya Mwl.Julius Nyerere barabara ya kilwa Temeke, jijini Dar es salaam.

Katika maonesho hayo ya kimataifa yaliyohitimishwa tarehe 13 Julai, 2022 na Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Philip Isdory Mpango,  amezitaka taasisi zinazowezesha biashara nchini ikiwemo BRELA kufanya kazi Kwa weledi ili kufungua milango ya uwekezaji nchini na kupunguza vikwazo kwa wawekezaji. 

Katika hafla hiyo Makamu wa Rais Dkt.Mpango amezitaka taasisi zinazowezesha biashara nchini kujituma na kufungua milango ya kibiashara baina ya Tanzania na mataifa ambayo bado hayajafikiwa, ili kuongeza wigo wa kibiashara kwa wawekezaji  na Taifa kwa ujumla.

Ameongeza kuwa Wizara zinazohusika na masuala ya uwekezaji zifungue mipaka kwa kutatua changamoto zinazowakazwa wawekezaji, huku akiwataka wafanyabiashara kuwa wawazi kuelezea kinachowatatiza ili kifanyiwe kazi kwa haraka na hatimaye kuondoa vikwazo.

“Niwaombe taasisi za Serikali na taasisi binafsi kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuondoa changamoto zilizopo na kufungua milango ya uwekezaji, lakini pia nanyi wafanyabiashara muwe wawazi  kwa kueleza ni nani anawakwamisha ili tuyashughulikie Kwa haraka,” ameongeza Dkt. Mpango.

Pia amezitaka taasisi za Fedha kuwawezesha kiuchumi wawekezaji, ili kupata mitaji kwani janga la uviko-19 lilisababisha biashara nyingi kuyumba.

Maonesho ya 46 ya Biashara kimataifa ya Da es Salaam, yalianza tarehe 28 Juni, 2022.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here