Home BUSINESS WABUNIFU KUONA MATUNDA YA BUNIFU ZAO KUPITIA BRELA

WABUNIFU KUONA MATUNDA YA BUNIFU ZAO KUPITIA BRELA

Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) imewataka wabunifu kusajili Bunifu zao BRELA  ili kuona matunda ya kazi zao.

Akizungumza katika Warsha ya Miliki Ubunifu katika chuo  Chuo Cha Don Bosco jijini  Arusha leo tarehe 16 Juni, 2022, Afisa Sheria kutoka Idara ya Miliki Ubunifu Bw. George Msaki amesema imefika wakati kila   mbunifu aone matunda ya anacho kifanya kwa kujisajili BRELA.

Amesema ana imani kuwa elimu ya Miliki Ubunifu wanayoitoa vyuoni italeta chachu kwa watalam kuendelea kuvumbua na kumiliki kisheria bunifu zao kwa ajili ya maendeleo binafsi na Taifa kwa ujumla.

“Vumbuzi nyingi zipo vyuoni ndiyo maana tukaanzia huku kutoa elimu hii, tunaamini mmeelewa na matokeo  yataonekana kupitia ongezeko  la usajili,” amesema Bw.Msaki

Amewasihi pia wanafunzi hao kurasimisha biashara zao kupitia Mfumo wa Usajili kwa njia ya Mtandao unaojulikana kama ORS.

Bw. Msaki amesema zoezi la utoaji elimu ya Miliki Ubunifu ni endelevu na litafanyika  nchi nzima.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here