MBUNGE wa Jimbo la Singida Magharibi Elibariki Kingu ametembelea eneo la miradi itakapojengwa Shule Shikizi katika KijijiK cha Masweya Kitongoji cha Nsonga Ndogowilayani Ikungi mkoani Singida ambapo aliwakilishwa na Katibu wake Abubakar Muna.
Katika ukaguzi huo uliofanyika mwishoni mwa wiki, Muna kukutana na viongozi wa Halmashauri ya Kijiji cha Masweya na baadhi ya viongozi wa chama kutoka kwenye matawi yote matatu na kuzingumza nao.
Mazungumzo mkubwa yaliyofanyika baina yao yalihusu maendeleo ya miradi minne inayotekelezwa katika maeneo mbalimbali kwenye vitongoji vya Ifyamahumbi ambao wanamradi wa madarasa mawili yanayoendelea kujengwa.
Akizungumza na waandishi wa habari Muna alisema miradi yote inayotekelezwa katika maeneo hayo unakwenda vizuri kutokana na ushirikiano mkubwa wa wananchi na viongozi.
Alisema katika Kitongoji cha Nsonga Ndogo wana mradi wa Shule Shikizi ambapo walipewa mifuko 100 ya saruji na Mbunge Elibariki Kingu huku Sh. 50 Milioni zikitolewa na Rais Samoa Suluhu Hassan kwa ajili ya akisaidia ujenzi wa Zahanati ya Kitongoji hicho.
Alisema ujenzi wa mradi wa Zahanati wa Kitongoji cha Masweya unaendelea vizuri na umefikia hatua
ya lenta.Nsonga Ndogo iliopewa mil 50 na Mh Rais mama Samia Suluhu Hassan,mradi wa mwisho ni zahanati ya Masweya ilioko kwenye lenta.
Muna alisema wananchi wa vitongoji vyote pamoja na viongozi wao wamekubaliana kuendelea na miradi kwakuchangia kila kaya ili kuisukuma mbele miradi hiyo na kuhakikisha inakamilika ikiwa ni kuunga mkono jitihada za mbunge wao Viongozi pamoja na wananchi wameridhishwa na utekelezaji wa miradi hiyo wakatumia nafasi hiyo kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwapa fedha na pia wakampongeza Mbunge wao Kingu kwa kazi nzuri huku wakihimiza kudumisha ushirikiano baina yao.