Home BUSINESS TRA YATANGAZA MSAMAHA WA RIBA NA ADHABU KWA WAMILIKI WA VYOMBO VYA...

TRA YATANGAZA MSAMAHA WA RIBA NA ADHABU KWA WAMILIKI WA VYOMBO VYA MOTO VILIVYOINGIZWA NCHINI KINYUME CHA SHERIA

Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Umma (TRA) Richard Kayomboa akizungumza katika mkutno na waandishi wa habari kuhusu msamaha wa riba na adhabu kwa wamiliki wa vyombo vya moto. Mkutano huo umefanyika leo katika ofisi za mamlaka hiyo Jijini Dar es Salaam.


Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Umma (TRA) Richard Kayombo (kushoto) akizungumia hatua aliyochukua Kamishna Mkuu wa TRA kuhusu kutoa msamaha huo. (kulia) ni Meneja msaidizi Udhibiti na Ushurutishaji wa mamlaka hiyo John Micah.


Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Umma (TRA) Richard Kayomboa (kushoto) akizungumza katika mkutno na waandishi wa habari leo april 25,2022 kuhusu msamaha huo. (katikati) ni Meneja msaidizi Udhibiti na Ushurutishaji wa mamlaka hiyo John Micah, na (kulia) ni Afisa Forodha wa TRA Frolah Tutu.


Maofisa wa TRA wakifuatilia mkutano huo, (kushoto) ni Julieth Kidemi Afisa msimamizi wa Kodi na (kulia) Afisa forodha Mkuu (Principal Customs Officer) Michael Kasongwa.


Waandishi wa habari kutoka katika vyombo mbalimbali wkifuatilia mkutano huo. (PICHA ZOTE NA: HUGHES DUGILO)

Na:Hughes Dugilo, DAR ES SALAAM.

Mamlaka ya Mapato TRA imetangaza msamaha wa riba na adhabu kwa wamiliki wa vyombo vya moto vilivyoingizwa nchini kinyume cha sheria ikiwa ni sehemu ya kutoa motisha kwa walipa kodi hao kujitokeza kulipa kodi kwa hiari na wakati.

Akitangaza msamaha huo mbele ya waandishi wa habari Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Umma (TRA) Richard Kayombo amesema kuwa msamaha huo unahusisha vyombo vilivyoingizwa kwa njia zisizo rasmi, vyombo vilivyokusudiwa kwenda nchi jirani lakini vikaingizwa nchini kinyume cha utaratibu, vilivyoingizwa nchini kwa muda na kuzidisha muda wa kukaa nchini (Temporary importation) na vilivyotumia msamaha wa kodi kinyume na sheria au kubadilishiwa umiliki bila kufuata utaratibu.

Kayombo, mefafanua kuwa masamaha huo umetolewa kwa mujibu wa kifungu cha sheria namba 70 (2) cha Sheria ya usimamizi wa kodi ya mwaka 2015, kama ilivyofanyiwa marekebisho na sheria ya Fedha ya mwaka 2021 pamoja na kifungu cha 249 cha Sheria ya usimamizi wa Ushuru wa Forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya mwaka 2004 ambazo zinampa Kamishna Mkuu wa TRA mamlaka ya kusamehe riba na adhabu.

“Msamaha huu umelenga kujenga ushirikiano na uhusiano mwema kati ya TRA na walipakodi hao, kuwapa motisha ya kulipa kodi kwa hiyari na wakati, pamoja na kuweka kumbukumbu au taarifa sahihi za umiliki wa vyombo hivyo” amesema Kayombo.

Aidha TRA imetoa wito kwa wamiiki wote wa vyombo hivyo vya moto kujitokeza ndani ya muda wa msamaha uliotolewa na Kamishna Mkuu ili waweze kulipa kodi halisi inayodaiwa na kuweza kukomboa vyombo vyao. 

MWISHO.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here