Home BUSINESS NMB YAGEUKIA WAKULIMA, YAMWAGA MABILIONI KWA RIBA NAFUU

NMB YAGEUKIA WAKULIMA, YAMWAGA MABILIONI KWA RIBA NAFUU

Afisa Mkuu Wateja Binafsi na Biashara wa NMB, Filbert Mponzi (kushoto) akitoa maelezo kwa Rais Samia Suluhu Hassan alipotembelea banda la NMB kwenye uzinduzi wa ugawaji wa vitendea kazi kwa maafisa Ugani Kilimo Nchini uliofanyika jana Jijini Dodoma. Benki ya NMB ni wadhamini wa Hafla Hiyo na wadau wa kuliko. Pembeni ya Rais ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

JUMLA ya Sh78.8 bilioni zimeshatolewa na benki ya NMB kwa wakulima kati ya Sh100 bilioni walizotengewa kwa ajili ya kukopeshwa kwa riba nafuu ili kusaidia kukuza mnyororo wa kilimo.

Fedha hizo ni sehemu ya mkakati wa benki ya NMB kwa ajili sekta ya kilimo inayoajiri watanzania wengi zaidi ambapo benki inatoa fedha hizo kwa riba isiyozidi asilimia 10.

Takwimu hizo zilitolewa jana na Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara Filbert Mpozi wakati akimkaribisha Rais Samia Suluhu Hassan alipotembelea banda la benki hiyo kubwa nchini.

Kwa upande wake Rais alipongeza juhudi zote zinazofanyika ndani ya benki hiyo akisema kuwa anawashukuru sana kwa juhudi zao hizo.

Rais alifika katika banda hilo kwenye hafla ya ugawaji wa vitendea kazi kwa Maafisa Ugani nchi nzima ambayo ilifanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma.

Mponzi alisema Kati ya shilingi bilioni 100 zilizotengwa kukopeshwa kwa wakulipa kwa riba ya chini ya asilimia 10, zaidi ya shilingi bilioni 78.8 zimeshakopeshwa kwa wanufaika 3,773 huku wakiwafikia zaidi ya wakulima na wajasiliamali wa kilimo milioni 1.4 kupitia taasisi yao ya NMB Foundation.

“Mbali na kiwango hicho, pia benki ya NMB imefanikiwa kuandaa mpango wa kufungulisha akaunti kwa wakulima, wavuvi na wafugaji ambapo katika kipindi cha miaka miwili iliyopita zaidi ya akaunti 500,000 zilifunguliwa,” alisema Mponzi.  Afisa huyo alisema lengo la njia hiyo ni kuwawekea wakulima utaratibu maalumu ili wakidhi vigezo vya kupatiwa huduma za kifedha ikiwemo mikopo na mafunzo.

Kwa mujibu wa Afisa huyo, mpango huo ni kuunga juhudi za serikali, katika kusukuma mbele agenda ya maendeleo ya kiuchumi ya Vijana na Wanawake, hivyo waliamua kutangaza hati fungani maalumu tuliyoiita waliyoiita JASIRI BOND.

Hati hiyo imejikita katika kuwasaidia kusaidia wanawake wajasiliamali kwa riba nafuu ambapo mwitikio umekuwa mkubwa sana hata wameamua kuzindua NMB PESA lengo likiwa ni kurahisisha huduma za kipesa kwa wakulima na wateja wote kuwa karibu zaidi kwenye maeneo yao.

Akizungumzia utoaji wa mbegu za mafuta alisema tayari wateja 332 wakiwemo wakulima katika vyama vya ushirika (AMCOS) wameshanufaika na zaidi  Sh 6 bilioni  zimetolewa kwenye eneo hilo kama mikopo.

Nyingine ni kuwa benki hiyo imeshatoa zaidi ya Sh110 milioni kama mikopo ya bima ya afya za afya kwa makundi na taasisi za wakulima 697.

Baada ya juhudi za Serikali kutangazwa katika kuongeza uzalishaji wa Mafuta nchini na kupunguza kiasi cha fedha kinachotumika kuagiza Mafuta nje, NMB wameshafanya mawasiliano na wizara ya kilimo ili kuunga mkono juhudi hizo na tayari wametengeneza muundo wa mikopo kwa wakulima na mnyororo thamani unaeleza jinsi ya kuwasaidia wakulima.

Kwenye sekta ya mikopo NMB kwa kipindi cha miaka mitano wameshakopesha zaidi ya Sh1.3 trilioni kwenye kilimo, uvuvi na ufugaji na minyoyoyo yote ya thamani. Kingine ni kuwa, wameshaandaa mpango wa kufungulisha akaunti kwa wakulima, wavuvi na wafugaji ambapo kwa miaka miwili iliyopita, zaidi ya akaunti 500,000 zilifunguliwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here