|
Na: Heri Shaaban
MUFT wa Tanzania Abubakar Bin Zuberi, ameongoza Wana nchi wa Wilaya ya Ilala katika Dua Maalum ya kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan katika utekelezaji wa Ilani na majukumu yake ya kazi
MUFT Bin Zuberi aliongoza Dua hiyo ya Wananchi wa Wilaya ya Ilala katika futari Maalum iliyoandaliwa na Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Omary Kumbilamoto katika ukumbi wa Karimjee Wilayani Ilala.
Muft Zuberi alisema Leo ni siku Maalum kwa Wananchi wa Halmashauri ya Jiji katika futari hii ya Meya wa Halmashauri ya Jiji kuwafuturisha Wananchi wake .
“Nyoyo za Wanadamu zimeumbwa kwa ajili ya kupeana mambo mema umoja huu na mshikamano wa Ilala uendelee kudumu uwe endelevu pamoja na kumuombea Dua Rais wetu Samia Hassan Suluhu nakuombea Dua Meya Omary Kumbilamoto pamoja na Mkurugenzi Jumanne Shauri Mwenyezi Mungu awabariki katika utekelezaji wa majukumu yenu ya kazi Mwenyezi Mungu awaondolee na KERO alisema
Kwa upande wake Katibu Tawala mkoa Dar es Salaam Hassan Lugwa, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam aliwashukuru Halmashauri ya Jiji kwa kuwafursha Wananchi ni jambo kubwa kwa Ustawi wa Jamii na Taifa kwa ujumla.
Katibu Tawala mkoa Dar es Salaam Hassan ,alipongeza mshikamano wa Wilaya ya Ilala ametaka uwe endelevu katika juhudi za kumsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mkurugenzi wa AL Hikima Nurudin Kishik alisema Meya Kumbilamoto amefanya jambo jema katika kuwafurisha Wananchi na kujenga mahusiano mazuri na Wananchi wake.
Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Omary Kumbilamoto alimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TANZANIA kwa kumpatia shilingi milioni 400 kwa ajili ya Malipo ya wastaafu wa Wilaya ya Ilala wote ambapo wote wamelipwa
Mwisho