Home BUSINESS MHE CHANA: ROYAL TOUR NI LANGO KUU LA FURSA KATIKA UTALII

MHE CHANA: ROYAL TOUR NI LANGO KUU LA FURSA KATIKA UTALII

Waziri wa Maliasili na Utalii nchini Mhe Balozi Dkt Pindi Chana akiwasili Katika Kiwanja Cha Ndege Cha Kimataifa Kilimanjaro -KIA.

Waziri wa Maliasili na Utalii nchini Mhe Balozi Dkt Pindi Chana akifanya mahojiano na Mwandishi  wa habari baada ya kuwasili Katika Kiwanja cha  Ndege Cha Kimataifa Kilimanjaro -KIA

Waziri wa Maliasili na Utalii nchini Mhe Balozi Dkt Pindi Chana akikagua maandalizi ya ukumbi utakaohusika Katika Uzinduzi wa Filamu ya Royal Tour.

 Waziri wa Maliasili na Utalii nchini Mhe Balozi Dkt Pindi Chana akishiriki katika Maandalizi ya kuelekea uzinduzi wa Filamu ya Royal Tour.


Waziri wa Maliasili na Utalii nchini Mhe Balozi Dkt Pindi Chana akizungumza jambo na Msanii wa Muziki wa mashairi Nchini Mrisho Mpoto.


Waziri wa Maliasili na Utalii nchini Mhe Balozi Dkt Pindi Chana, ametoa wito kwa watanzania kukaa tayari kwa kuchangamkia furusa mbalimbali zitakazo tokana na matokeo chanya ya Filamu ya Royal Tour inayo tarajiwa kuzinduliwa Jijini Arusha.
 

Mhe Chana ameyasema hayo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro, alipo wasili tayari kuudhuria uzinduzi wa Filamu hiyo muhimu kwa sekta ya Utalii nchini.
 

“Royal Tour Arusha inakwenda kufungua zaidi furusa za Utalii nchini, Mhe Rais wetu Mpendwa Mama Samia Suluhu Hassan ametufungulia furusa hii, sasa sote tukae katika mkao wa kunufaika nayo” Mhe Chana.
 

Na katika hatua nyingine Mhe Chana amekagua ukumbi wa utakaotumika kuzindulia Filamu hiyo na kuridhishwa na maandalizi hayo.
 

‘Filamu ya Royal Tour inatarajiwa kuzinduliwa Jijini Arusha hapo kesho

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here