Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Bwa. Kaspar Mmuya (katikati) akiongoza Kikao cha Kamati ya Makatibu Wakuu ya Kuratibu Utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano Dhidi ya UVIKO-19 (mwisho) Mkurugenzi Idara ya Menejimenti ya Maada Ofisi ya Waziri Mkuu Meja Jenerali Michael Mumanga na (wa kwanza kulia) Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Elias kikao kilichofanyika Ukumbi wa Ofisi hiyo Aprili 25, 2022 Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Zainab Chaula akieleza jambo wakati wa kikao cha Kamati ya Mkatibu Wakuu ya Kuratibu Utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano Dhidi ya UVIKO-19 kilichofanyika Ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Aprili 25, 2022 Dodoma.
Baadhi ya washiriki kutoka Wizara mbalimbali wakifuatilia kikao hicho kilichofanyika Ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Aprili 25, 2022 Dodoma.
(PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
(SERA, BUNGE NA URATIBU)
Na Mwandishi Wetu- Dodoma
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Kaspar Mmuya ameongoza Kikao cha Kamati ya Makatibu Wakuu ya Kuratibu Utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano Dhidi ya UVIKO-19.
Kikao hicho kilifanyika Aprili 25, 2022 Dodoma ambapo Makatibu Wakuu na Wawakilishi kutoka Wizara mbalimbali walishiriki kikao hicho zikiwemo Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Wizara ya Kilimo, Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) na nyinginezo.
MWISHO